Ruto amewaeleza wajumbe wanaojumuisha wakuu wa nchi, watunga sera, viongozi wa serikali, watoa maamuzi, wataalam wa mabadiliko ya tabianchi, mashirika ya kimataifa na mashirika ya kiraia, na sekta binafsi kuwa wakati umefika sasa wa bara la Afrika kutafuta ufumbuzi wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa barani Afrika.
Ruto, kando na kuwataka viongozi wa Kiafrika na kimataifa, wafuatiliaji wa uvumbuzi, wataalam, wawekezaji, na wakuu wa tasnia mbalimbali kulitumia jukwaa hili kama ukumbi wa majadiliano kuchunguza mawazo, kutathmini mitazamo, na kufungua masuluhisho kwa siku tatu zijazo, amewarai wajumbe kubuni mkakati wa kubadilisha utajiri wa rasilimali za Afrika kutoka kwa uwezo hadi kuwa fursa halisi, kwa kuelekeza uwekezaji mkubwa ambao utafanikisha uwezekano uliopo kuvinufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.