Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:38

HAYATI BENJAMIN MKAPA : SAFARI NDEFU YA MWANADIPLOMASIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ametangaza kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 24 Julai, 2020.

Rais Magufuli amesema Benjamin William Mkapa amefariki dunia hospitalini Jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Rais Magufuli amewataka Watanzania kuwa watulivu na wastahimilivu baada ya kupokea taarifa za kuondokewa na mpendwa wao Benjamin William Mkapa.
“Kwa masikitiko makubwa tumepata msiba mkubwa, Mzee wetu Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu amefariki dunia, amefariki dunia katika hospitali Jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa, niwaombe Watanzania tulipokee hili, tumepata msiba mkubwa na tuendelee kumuombea Mzee wetu Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa ambaye ametangulia mbele za haki, taarifa zingine zitaendelea kutolewa lakini Mzee Mkapa hatunaye tena” amesema. Rais Magufuli katika taarifa yake kwa Taifa.
Yafuatayo ni matukio muhimu yaliyoko katika kumbukumbu ya mahusiano yake na viongozi wa ulimwengu na nafasi yake kama mwanadiplomasia...


Pandisha zaidi

16x9 Image

Jaffar Mjasiri

Ni Mwandishi na Msimamizi wa Mitandao ya Kijamii, VOASwahili

 

Makundi

XS
SM
MD
LG