Rais Magufuli amesema Benjamin William Mkapa amefariki dunia hospitalini Jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
“Naamini mtoto wangu alifungua mlango wakati ule, miaka 21 iliyopita,” ukatili wa polisi na ubaguzi wa rangi kuchunguzwa, amesema mama huyo.
Maafisa wa Palestina wameupinga mpango wa Israel na kuikosoa Marekani baada ya utawala wa Rais Donald Trump kuiunga mkono Israeli kuchukuwa ardhi katika mpango wa amani uliotolewa mwezi Januari.
Tunda amekwaruzana na Rais Felix Tshisekedi juu ya mabadiliko ya mahakama yaliyopendekezwa na chama cha Tunda ambayo yataipa wizara ya sheria udhibiti zaidi juu ya uendeshaji wa kesi za jinai.
Kurejewa kwa uchaguzi kulionekana na wachambuzi kama ni jaribio la uwezo wa mahakama za Afrika kutatua suala la wizi wa kura na kudhibiti madaraka ya rais.
Watu wengine watatu walikuwa wamejeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo katika uwanja wa Bustani ya Forbury mjini Reading,
Ghebreyesus amesema Jumatatu tishio kubwa hivi sasa sio virusi vyenyewe, lakini hasa “ ni ukosefu wa mshikamano wa kimataifa na uongozi.”
Hatua hiyo inafuatia kujiuzulu Jumamosi kwa Mkuu wa Polisi wa mji wa Atlanta Erika Shields, baada ya Rayshard Brooks, umri miaka 27, kuuawa Ijumaa
Afisa wa polisi mjini Atlanta afukuzwa kazi baada ya kupiga risasi iliyosababisha kifo cha mtu mweusi na afisa mwengine amepangiwa kazi nyingine za kiutawala, idara ya polisi imetangaza mapema Jumapili
Barua hiyo iliyosainiwa na nchi 54 imeandikwa na Balozi wa Burkina Fasoka katika Umoja wa Mataifa kwa niaba yao.
Tarhouna ilikuwa ngome ya muasi Jenerali Khalifa Haftar na vikosi vyake, lakini hivi karibuni ilikombolewa.
Rais wa Russia Vladimir Putin alisema kama kuna raia wa Russia nchini Libya, hawako kuiwakilisha serikali ya Russia, na wala hawalipwi na serikali yake.
Maafisa wote wanne wamewekwa rumande na kufukuzwa kazi idara ya polisi.
Nchini Ujerumani, waandamanaji walibeba ujumbe unaosema, “Wawajibisheni Askari,” na “Nani Unamwita Wakati Polisi Anapouwa?”
Kampuni ya Netflix ilituma ujumbe wa tweet “kukaa kimya ni kuunga mkono uhalifu,” ikiongeza kuwa “tuna wajibu kwa washiriki, wafanyakazi, watengenezaji na vipaji wetu Weusi kupaza sauti.
Waziri Mkuu wa Canada : “Ubaguzi uko. Uko nchini Marekani, lakini pia uko Canada. … Tunafahamu watu wanakabiliwa na mfumo wa ubaguzi, kuegemea upande mmoja na ubaguzi dhidi ya watu weusi bila ya kujitambua kila siku.
Maandamano yamefanyika katika miji mbalimbali duniani Jumamosi, ikiwa ni mshikamano wa namna fulani na waandamanaji wa Marekani kufuatia kifo cha Mmarekani mweusi wakati akiwa mikononi mwa polisi mapema wiki hii.
“Ninatatizwa sana na kifo kibaya cha George Floyd huko Minneapolis...Vikosi vya usalama duniani ni lazima viwajibishwe. Hakuna yeyote aliyekuwa juu ya sheria.”
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo na Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi wamepinga sheria mpya ya usalama ya China inayoshinikizwa Hong Kong.
Video hiyo inaonyesha afisa mzungu akikandamiza shingo ya Floyd kwa goti lake ambaye tayari alikuwa amefungwa pingu.
Pandisha zaidi