Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:46

UN kusaidia uchunguzi wa makaburi ya jumla nchini Libya


Mwanajeshi wa jeshi la utawala wa Libya unaotambulika kimataifa akionyesha makaburi ya pamoja yaliogunduliwa Tarhouna , Libya, Juni 11, 2020.
Mwanajeshi wa jeshi la utawala wa Libya unaotambulika kimataifa akionyesha makaburi ya pamoja yaliogunduliwa Tarhouna , Libya, Juni 11, 2020.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anasema katibu mkuu “ameshtushwa sana na habari za kugunduliwa makaburi ya jumla katika siku za karibuni, mengi kati ya hayo katika mji wa Tarhouna” nchini Libya.

Tarhouna ilikuwa ngome ya muasi Jenerali Khalifa Haftar na vikosi vyake, lakini hivi karibuni ilikombolewa.

Msemaji wa Guterres, Stephane Dujarric anasema mkuu wa UN ameamuru “uchunguzi wa kina na wa uwazi ufanyike, na waliotenda uhalifu huo kufikishwa mbele ya sheria.

Guterres pia ametoa msaada wa UN, Dujarric anasema, “ kufukua makaburi hayo, kuwatambua waathirika, kuchunguza sababu za vifo vyao na kukabidhi miili hiyo kwa familia zao.”

Philippe Nassif, mkurugenzi wa shirika la kutetea haki (Amnesty International) kwa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, ameliambia shirika la habari la Associate Press kuwa alitaka taasisi yake au UN “ kwenda Libya na kukusanya ushahidi juu ya kufanyika kwa jinai ya kivita na mauaji mengine … ili hatimaye mchakato ufanyike kutafuta haki kwa wale waliodhulumiwa.

Tarhouna iko kilomita 65 kusini mashariki ya mji mkuu wa Libya, Tripoli.

XS
SM
MD
LG