Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:51

UN yasema wahamiaji 400 wamekamatwa nje ya pwani ya Libya


Moshi unaotokana na shambulizi katika bandari ya Tripoli, Libya Februari 18, 2020. REUTERS/Ahmed Elumami
Moshi unaotokana na shambulizi katika bandari ya Tripoli, Libya Februari 18, 2020. REUTERS/Ahmed Elumami

Walinzi wa pwani ya Libya wamekamata wahamiaji 400 waliokuwa wakonjiani katika pwani ya Mediterranean ya nchi hiyo wakielekea Ulaya na kuwarejesha katika mji mkuu wa Tripoli masaa 24 yaliyopita, Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa UN limesema Jumapili.

Shirika la Habari la Associated Press limesema Shirika la Kimataifa la Wahamiaji limetuma ujumbe wa tweeter likieleza wahamiaji 301 wakiwa katika boti tatu walikamatwa Jumamosi na kurejeshwa mjini Tripoli. Wahamiaji wengine 105 wakiwa katika boti mbili walitiwa nguvuni Jumapili.

Shirika hilo limesema wengi kati ya wahamiaji hao wamewekwa rumande mbalimbali mjini Libya, ambako kuna “wasiwasi mkubwa juu ya usalama wao.”

Baadhi ya wahamiaji walifanikiwa kukimbia walipofika sehemu ya kushuka, boti hizo zilipokuwa zinapelekwa ufukoni, IOM imesema.

“Hili halikubaliki kuendelea kutokea pamoja na kuwepo wito kuacha kabisa kuwarejesha watu walioko hatarini vizuizini na kufanyiwa vitendo vya viovu,” amesema Safa Msehli, msemaji wa IOM.

Libya iliingia katika machafuko kufuatia machafuko ya 2011 yaliyopelekea kupinduliwa na kuuawa kwa kiongozi wa kiimla Moammar Gadhafi, na kuwa ni kituo kikuu cha wahamiaji Waafrika na Waarabu wanaokimbia vita na umaskini wakielekea Ulaya.

Wahamiaji wengi wanafanya safari kwa kutumia maboti yasiokuwa salama yaliyotengenezwa kwa mpira. Shirika la IOM limesema mapema mwezi huu inakadiria vifo vya wahamiaji waliojaribu kuvuka bahari ya Mediterranean imevuka na ilivuka “idadi ya kutisha” ya watu 20,000 tangu mwaka 2014.

Katika siku za hivi karibuni, Umoja wa Ulaya imeendelea kushirikiana na walinzi wa pwani na vikosi vingine vya Libya kuzuia kuingia kwa wahamiaji.

Makundi yanayopigania haki za kibinadamu yanasema kuwa juhudi hizo za kuzuia wahamiaji zimewaacha katika mikono ya makundi ya ukatili yenye silaha au kuishia kuweka katika vizuizi vyenye hali mbaya ya usafi na zenye msongamano mkubwa wa watu visivyokuwa na chakula na maji.

Umoja wa Ulaya mapema mwaka huu umekubali kusitisha operesheni dhidi ya wavushaji wa wahamiaji haramu inayohusisha ndege zenye kufanya doria na badala yake watapeleka meli za kivita kujikita katika kuhakikisha vikwazo vipana vya uingizaji silaha vinatekelezwa ambavyo vinakadiriwa ni muhimu kumaliza vita vinavyoendelea nchini Libya.

XS
SM
MD
LG