Watu hao waliuawa kutokana na mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari mjini Benghazi, mashariki ya nchi hiyo.
Shambulio hilo la Jumamosi asubuhi limetokea wakati UN inajaribu kutafuta suluhisho la kusitisha mapambano yaliyoanza mwezi Aprili katika mji mkuu wa Tripoli.
Mapiganao hayo yalianzishwa na wanamgambo national Army wenye makazi yao mashariki ya nchi ya Libya, yakiongozwa na Jenerali aliyeasi Khalifa Haftar yakiwa na lengo la kuipindua serikali inayotambuliwa na UN, na mpaka sasa mapinduzi hayo hayajafanikiwa.
Baraza la Usalama la UN lilikutana katika kikao cha dharura jana kujadili suala la Libya.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.