Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 15:31

Libya yakanusha kuwatelekeza wanawake, mtoto baharini


Wahamiaji waliokolewa wakiwa katika boti ya shirika la Proactive Open Arms.
Wahamiaji waliokolewa wakiwa katika boti ya shirika la Proactive Open Arms.

Walinzi wa pwani ya Libya wamekanusha tuhuma zilizotolewa na kikundi cha msaada cha Spain kwamba waliwatelekeza wanawake wawili na mtoto wafie kwenye bahari ya Mediterranean.

Msemaji wa walinda doria Ayoub Gassim Jumanne amesema shughuli zao ni kuwaokoa wahamiaji wanaokuwa safarini kuelekea Ulaya, “kwa mujibu wa viwango vya kimataifa vinavyofuatwa katika kuokoa maisha ya watu baharini.”

Aliwalaumu wasafirishaji wa binadamu na “na kutowajibika kwa makundi yasiyo ya serikali” kwa maafa yote yanayotokea baharini.

Amesema walinzi wa pwani ya Libya walikamata Jumatatu boti iliyokuwa inaelekea Ulaya ikiwa na abiria 160.

Lakini kikundi cha Spain kinachoitwa Proactive Open Arms, kimesema Jumanne kilimkuta mwanamke mmoja akiwa hai na mwengine amekufa, pamoja na mwili wa mtoto, uliokuwa ndani ya boti ya mpira nje ya pwani ya Libya.

Mkuu wa kikundi cha Proactive Open Arms, Oscar Camps amesema wanawake hao wawili walikataa kupanda boti za Libya zilizokuwa na wahamiaji wenzao na waliachwa baharini baada ya walinzi wa pwani ya Libya kuiharibu boti yao.

Camps pia ameilaumu serikali mpya ya Itali iliochaguliwa kwa umaarufu juu ya vifo vya wahamiaji baada ya kuapa kwamba itazuia wahamiaji wanaovuka bahari ya Mediterranean na imevipa msaada vyombo vya usalama vya Libya kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa wakala wa wahamiaji wa Umoja wa Mataifa zaidi ya wahamiaji 1,400 wamekufa au hawajulikani waliko baada ya kujaribu kuvuka bahari ya Mediterranean hadi Julai 15, 2018.

XS
SM
MD
LG