Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:04

UN yaomba mamlaka Libya kuwadhibiti wahamiaji


Wahamiaji wakiwa katika boti Open Arms iliowaokoa ikiwasili Barcelona, Spain, Wednesday, Julai 4, 2018.
Wahamiaji wakiwa katika boti Open Arms iliowaokoa ikiwasili Barcelona, Spain, Wednesday, Julai 4, 2018.

Mkuu wa idara ya Umoja wa Mataifa inayohusika na uhamiaji, William Lacy Swing ameiomba mamlaka nchini Libya kuwatia ndani wahamiaji wanaokamatwa baharini na walinzi wa pwani wakati wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean kwenda Ulaya

Shirika la kimataifa la uhamiaji (IOM) limeipongeza Libya kwa kuzidisha juhudi za kupambana na operesheni za wanaofanya magendo ya kusafirisha watu. Kwa msaada wa Umoja wa Ulaya, inaeleza kuwa idadi ya wahamiaji waliookolewa kwenye maji ya Libya na kurejeshwa ufukweni imeongezeka kwa idadi kubwa.

Msemaji wa IOM, Leonard Doyle anasema katika mwezi mmoja uliopita pekee, walinzi wa pwani wa Libya wameweza kuwapata takriban wahamiaji 4,000 waliokuwa wakisafiri kwenda Ulaya,

“Licha ya kile tunachokifahamu kuna mambo ya kihuni, kwa ujumla inaonekana kuna azma ya walinzi wa pwani kuokoa maisha ya watu, kuwarejesha kwenye nchi zao kila inapowezekana na kuepusha uhamiaji holela na majanga ambapo watu pekee wanaonufaika na hili ni wafanya magendo,” anasema Doyle.

Mkuu IOM, Swing hivi karibuni alirejea katika ziara ya siku mbili nchini Libya ambako aliiomba mamlaka ya kuondoa sera za kikatili za kuwatia ndani wahamiaji ambao tayari wamepata maafa wakati wanapojaribu kufika kwenye fukwe za Ulaya. Doyle anasema kuna baadhi ya dalili kuwa mamlaka iko tayari kufikiria hili.

“Kwa hakika kama wakifanya hivyo kwa kujaribu kuharakisha kuwarejesha makwao. Tutawapa msaada wa kurejeshwa kwa hiari, kuondoka kwa hiari, kupata msaada wa kibinadamu kurejea Libya, inaweza kuchukua muda kwasababu hawana makaratasi, hawana nyaraka zinazohitajika. Ni ofisi za kibalozi katika nchi, balozi za kiafrika na pia hizo ni chache, anasema mkuu wa IOM.

Doyle anasema mara nyaraka na utaratibu wa rasmi utakapokamilika, itakuwa ni rahisi mno kuwarejesha wahamiaji, anasema IOM ina ndege za kukodisha ambazo zinakwenda kwenye mataifa ya Afrika karibu kila siku, huwachukua watu ambao wanataka kurejea nyumbani kwa hiari yao.

XS
SM
MD
LG