Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:09

UNHCR yaonya wahamiaji wataendelea kufa


Shirika lisilo la kiserikali limetangaza Jumamosi kuwa limewaokoa wahamiaji 59 kutoka Libya wakisafiri katika bahari ya Mediterranean, June 30, 2018.
Shirika lisilo la kiserikali limetangaza Jumamosi kuwa limewaokoa wahamiaji 59 kutoka Libya wakisafiri katika bahari ya Mediterranean, June 30, 2018.

Idara ya Umoja wa Mataifa ya kuhudumia wakimbizi ( UNHCR) inasema wahamiaji watarajiwa wataendelea kufa wanapojaribu kuvuka bahari ya Mediterranean kwenda Ulaya.

Idara hiyo inasema misimamo dhidi ya wahamiaji inakanganya juhudi za boti za kuokoa maisha.

Idara hiyo ya kuhudumia wakimbizi inasema watu wanao tafuta hifadhi na wahamiaji wanaendelea kuwasili Ulaya, wakati zaidi ya watu 1,000 wamefariki au kupotea baharini.

Pia imeongeza kuwa kiwango kikubwa cha watu wanaofariki kinaonyesha haja ya haraka kuimarisha msako na uwezo wa uokozi katika eneo hilo.

Lakini msemaji wa UNHCR, Charlie Yaxley anasema taasisi zisizo za kiserikali zinaweza kuwa na mchango mkubwa katika uokozi baharini na zinakatishwa tamaa katika kutoa misaada.

Yaxley ameiambia VOA ni muhimu kwamba meli yoyote ambayo iko karibu na boti zenye kutaka msaada ziruhusiwe kufanya hivyo.

Hivi karibuni, Italy na Malta zilikataa kuziruhusu boti zilizojaa wakimbizi na wahamiaji zilinyimwa ruhusu ya kutia nanga kwenye bandari zao, na kuzifanya boti hizo kukaa baharini kwa siku kadhaa.

Msimu wa safari za majaribio ya kuvuka bahari kwenda Ulaya ndiyo umeanza. Yaxley anasema kuokoa maisha lazima kiwe kipaumbele.

Ameonya kuwa kupunguza msako na juhudi za uokozi kutapelekea vifo zaidi, na wafanya magendo wasio na huruma wanawarubuni watu kuhatarisha maisha yao na kuvuka bahari kutumia boti hatarishi na zenye usalama duni.

XS
SM
MD
LG