Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:46

Afrika : Wahamiaji walio kwama baharini Libya wako hatarini


Meli ya Ujerumani inayo shughulika kuwatafuta na kuwaokoa wahamiaji baharini, Sea Watch 3, ikiwa imekwama kushusha wahamiaji baada ya Itali kukataa kuwapokea wahamiaji hao katika pwani ya Siracusa, Italy, Jan. 27, 2019.
Meli ya Ujerumani inayo shughulika kuwatafuta na kuwaokoa wahamiaji baharini, Sea Watch 3, ikiwa imekwama kushusha wahamiaji baada ya Itali kukataa kuwapokea wahamiaji hao katika pwani ya Siracusa, Italy, Jan. 27, 2019.

Wahamiaji kadha waliosalia ndani ya meli moja ya Ujerumani karibu na kisiwa cha Italy cha Sisiliya Jumapili walitoa wito kwa serikali wakiiomba iwaruhusu watuwe kwenye bandari hiyo.

Meli hiyo ya uokozi ilisafirisha wahamiaji 47 Januari 19 ikiwatoa kwenye bahari ya Libya.

Kufuatia hatua ya serikali ya Italy kukatalia boti za uokozi za watu binafsi, na hatua kama hiyo iliyo chukuliwa na viongozi wa kisiwa cha Malta, meli hiyo kutoka ujerumani ndio pekee inayofanya kazi ya kuwaokoa wahamiaji wanaokwama kwenye bahari ya Mediterraniani.

Kwa vile Meli hiyo imesimama karibu na kisiwa cha Sisiliya, haiwezi kwenda kuwaokoa wahamiaji ambao maisha yao yako hatarani karibu na Libya.

Meli hiyo iliruhusiwa kutua kwenye eneo la Italy kutokana na hali mbaya ya hewa, na kwa sababu serikali imekatalia mashirika ya misaada kuingia katika bandari za Italy, meli hiyo inaendelea kusimama kwenye umbali wa kilomita moja kutoka bandari ya sisiliya kwenye mjii wa mashariki wa Syracuse.

Jeshi la majini la Italy lilitowa msaada wa nguo, maji na chakula kwa wahamiaji hao 47 ambao bado wamesalia ndani ya meli hiyo ya uokozi kutoka ujerumani.

Jumapili, wabunge wa Italy waliingia ndani ya meli hiyo kukagua mazingira waliyomo wahamiaji hao. Wabunge wengi walibaini kuwa wahamiaji hao wameathirika kiakili na kimwili.

XS
SM
MD
LG