Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 03:56

Hofu ya msimamo mkali dhidi ya wahamiaji yaikumba Sweden


A photo taken on September 10, 2018 in Stockholm shows a selection of front pages of Swedish newspapers in Stockholm a day after the general elections.
A photo taken on September 10, 2018 in Stockholm shows a selection of front pages of Swedish newspapers in Stockholm a day after the general elections.

Matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa bunge Sweden uliofanyika Jumapili yanategemewa kutolewa baadae wiki hii, lakini matokeo ya awali yanaonyesha kuwa moja ya nchi za Ulaya zenye mrengo wa kiliberali zaidi ukifanya mabadiliko kwenda mrengo wa kulia na ikijishauri vipi itaunda serikali.

Wademokrati wa Sweden wenye kupinga uhamiaji ambao wanataka nchi hiyo kujitoa katika Umoja wa Ulaya na kuweka zuio la wahamiaji, inaelekea kuwa kitakuwa ni chama cha tatu kwa ukubwa katika bunge.

Wakati kura karibuni zote zikiwa zimehisabiwa, chama cha mrengo wa kushoto chenye msimamo wa wastani kinacho tawala cha Social Demokrats kina asilimia 28 za kura, kikifuatiwa na chama chenye msimamo wa kati, Moderates, kikiwa na asilimia 19 na chama cha nationalist Sweden Demokrats kikiwa na karibuni asilimia 18.

Vyama vya Social Demokrats na Moderates vimesema havitafikiria kuwa na muungano wa pamoja na chama cha Sweden Demokrats, kwani chama hicho kina mizizi ya sera za kinazi dhidi ya wahamiaji.

Chama cha Moderates kinasema kitaunda serikali ya mseto na kimemtaka Waziri Mkuu Stefan Lofven, ambaye ni wa chama cha Social Demokrat, kuachia madaraka.

Lofven amesema kuwa uchaguzi umeleta “hali ambayo vyama vyote venye kuwajibika ni lazima ikabiliane nayo,” na kuongeza kuwa “chama ambacho kinamizizi ya sera za kinazi” kamwe “hakitaweza kutoa kwa wananchi kitu chochote cha usimamizi, isipokuwa chuki tu.”

Kiongozi wa Sweden Demokrats Jimmie Akesson ametangaza ushindi katika mkutano uliohudhuriwa na wanao muunga mkono wakisema, “Sisi tutaweza kupata ushawishi mkubwa kutokana na yale yanayo tokea Sweden katika wiki, miezi na miaka ijayo.

Kabla ya uchaguzi, Lofven alikuwa ameonya, “Watu wenye chuki wana wahamasisha na kuchochea chuki kati ya watu nchini Sweden… Sisi tutapinga hilo. Tunasimama pamoja kutetea usawa.”

Sweden, kama ilivyo nchi nyingi za Ulaya, imekumbwa na wimbi la wanao omba hifadhi ya ukimbizi, ambao wengi wanakimbia kutoka Mashariki ya Kati, Asia ya Kusini na Afrika.

Wimbi hilo la wakimbizi 163,000 walio omba hifadhi nchini Sweden mwaka 2015, limewagawanya wapiga kura na kuvunja makubaliano mazuri yaliyokuwepo ya kisiasa.

Kura za maoni zilikuwa zimetahadharisha kuwa chama cha mrengo wa kulia cha Sweden Demokrats kingeweza kushinda kwa kura ya veto juu ya vyama ambavyo vitaweza kuunda serikali ijayo.

Magnus Blomgren, mtaalamu wa sayansi za kijamii katika chuo kikuu cha Umea, amesema, “Vyama vikongwe vimeshindwa kukabiliana na hisia hasi ambazo ziko hivi leo.”

XS
SM
MD
LG