Takriban wahamiaji 60 hawajulikani walipo, wakiaminika kwamba wamekufa maji baada ya boti walimokuwa wakisafiria kuzama baharini nchini Guinea-Bissau.
Walinzi wa baharini wamesema kwamba wameona boti hilo likielea katika bahari iliyokuwa imechafuka, lakini hawakuweza kuchukua hatua za haraka kuwaokoa waliokuwa kwenye boti hilo.
Mara nyingi, wahamiaji hutumia boti kwa safari yao kuelekea nchini uhispania kutoka mataifa ya Afrika magharibi.
Maafisa nchini Guinea Bissau wanasema kwamba wamefanikiwa kupata mabaki ya boti lakini hawajaweza kuokoa mtu yeyote wala kuopoa maiti.