Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 03:59

Idadi ya wakimbizi kutoka Afrika yashuka -Tafiti


Wakimbizi kutoka nchi za Kiafrika wanavyo hatarisha
maisha yao.
Wakimbizi kutoka nchi za Kiafrika wanavyo hatarisha maisha yao.

Marekani inaendelea kupokea idadi kubwa inayoongezeka ya wakimbizi wa Kikristo, hususan kutoka Afrika, ambapo idadi ya wale wanao wasili ikionekana kuwa iko chini kihistoria mwaka 2018, takwimu za serikali kuu zinaonyesha hivyo.

Wakati robo tatu ya mwaka wa fedha ukiwa umemalizika, na katikati ya hatua zinazoendelea za kubana matumizi kwenye programu ya wakimbizi kuja Marekani chini ya utawala wa Trump, takriban asilimia 68 ya wakimbizi wanaowasili katika mwaka huu wa fedha ni Wakristo.

Hata hivyo idadi hiyo kwa mwaka wa16 iko juu, kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iliyopitiwa na VOA.

Kabla ya mwaka huu, idadi kubwa ya wakimbizi hao ilikuwa mwaka wa fedha 2007, ikiwa ni asilimia 60.

Lakini watafiti na watetezi wa wakimbizi hao kwa haraka kabisa wamegusia kuwa wakati idadi ya wakimbizi Wakristo ikiwa juu kwa uwiano, idadi ya Wakristo, Waislam na watu wa dini nyingine iko chini ukilinganisha na miaka iliyopita.

“Sina taarifa ya Mkristo yoyote ambaye anafarijika kwa namna yoyote” kwa idadi hiyo iliyoko juu, amesema Mathew Soerens, mkurugunzi wa makanisa yanayo hamasisha misaada kwa dunia nzima, moja ya taasisi zinazoshughulikia kuwatufutia makazi wakimbizi nchini Marekani.

“Nafikiri ni msiba kwa Wakristo, Waislam na dini nyingine zote. Ukiangalia mengi ya makundi hayo kiwango cha wahamiaji wao imepungua kwa asilimia 60.

XS
SM
MD
LG