Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:20

Makao makuu ya jeshi maalum la Afrika lashambuliwa Mali


Wanajeshi wa Ufaransa wakiwa katika mafunzo nchini Mali
Wanajeshi wa Ufaransa wakiwa katika mafunzo nchini Mali

Washambuliaji wasiojulikana wamevamia makao makuu ya jeshi maaluma la Afrika katikati ya Mali siku ya Ijumaa, vyanzo vya ndani na vya Umoja wa Mataifa vimesema.

Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa juu ya kiwango au matokeo ya shambulizi hilo kwenye kambi ya kijeshi katika mji wa Sevare inayotumiwa na kikosi cha G5 Sahel, ambacho kiliundwa mwaka 2017 kutokomeza ghasia zinazoletwa na wanajihadi katika eneo la jangwa la Sahel huko Afrika Magharibi.

Kikosi cha G5 kinachoundwa na wanajeshi kutoka Mali, Niger, Burkina Faso, Chad na Mauritania, hawakujibu maombi ya kutoa maoni yao.

Katika miaka ya karibuni ghasia za wanamgambo wa kiislamu zimesambaa hadi kwenye eneo la Sahel ambalo ni wakazi wachache, makundi yenye uhusiano la Al Qaida na Islamic State wakitumia eneo la katikati na kaskazini mwa Mali kama ndiyo sehemu ya kufanyia mashambulizi kote katika eneo zima.

Mataifa ya magharibi, ikiwemo Ufaransa na Marekani, wametoa ufadhili mkubwa kwa G5 ikiwa ni juhudi za kuwashinda wanajihadi na kuondoa shinikizo kubwa kwa maelfu ya wanajeshi waliopelekwa katika eneo hilo.

Lakini jeshi hilo limekuwa na kasi ya pole pole kuanza kazi kwa nguvu, kutokana na uchelewesho wa fedha na uratibu miongoni mwa nchi tofauti.

Tume ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA) imekataa kusema chochote juu ya ripoti ya shambulizi.

XS
SM
MD
LG