Angalau mmoja wa washambuliaji hao alijilipua yeye mwenyewe ndani ya jengo hilo wakati wanamgambo wengine wakishambulia.
Kikundi cha Islamic State kimedai kuhusika na shambulizi hilo.
Libya imekumbwa na machafuko tangia kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Moammar Gadhafi alipopinduliwa na kuuwawa mwaka 2011.
Libya hivi sasa imegawanyika katika serikali mbili kinzani, kila moja ikisaidiwa na vikundi mbalimbali vya wanamgambo.
Serikali ambayo inatambuliwa kimataifa imeweka makao yake katika upande wa magharibi mwa Tripoli.
Hali hiyo ya kukosekana usalama imefungua milango kwa vikundi vya kigaidi kama vile IS kuweka kambi zao.