Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:29

Serikali ya Somalia yasema raia wake wamegoma kuondoka Libya


Ramani ya Libya ikipakana na Ulaya
Ramani ya Libya ikipakana na Ulaya

Juhudi za serikali ya Somalia kuwaondoa idadi kubwa ya wananchi wake kutoka Libya ziligonga ukuta baada ya ujumbe uliotumwa huko kushindwa kufanikisha zoezi hilo.

Kadhalika juhudi za kuwashawishi wahamiaji hao kuacha safari hatari za baharini kuelekea Ulaya na badala yake kurudi Somalia ziligonga mwamba.

Wajumbe hao wa Somalia walisema wahamiaji hao wamewaambia wamepata mateso wakati wa safari yao kwenda Libya na wanahisi hawana kingine cha kupoteza.

Vyanzo vya habari vimesema kuwa maafisa hao wanasema wahamiaji hao wa Somalia wameamua kufanya jaribio la mwisho kufikia kwenye fukwe za Ulaya.

Wajumbe wa mazungumzo waliofika Tripoli Jumatatu wamesema waametembelea kambi za kuwaweka watu kizuizini na pia wamepokea wahamiaji kutoka Ubalozi wa Somalia.

Lakini mpaka sasa ni watu 11 pekee walionyesha nia ya kutaka kurejea Somalia. Idadi ya raia wa Somalia ambao wamehamia Libya inakadiriwa kuwa kati ya 5000 hadi 6000, maafisa hao wamesema.

XS
SM
MD
LG