Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:17

Washukiwa wa al-Shabaab wauwa walimu watatu Kenya


Ponovno otvaranje kluba pod imenom "Klavir funkcioniše" u Londonu na Dan slobode kada se očekuje ukidanje gotovo svih ograničenja zbog korone virusa u Engleskoj. 19. juli, 2021. ( Foto: Alberto Pecali / AP )
Ponovno otvaranje kluba pod imenom "Klavir funkcioniše" u Londonu na Dan slobode kada se očekuje ukidanje gotovo svih ograničenja zbog korone virusa u Engleskoj. 19. juli, 2021. ( Foto: Alberto Pecali / AP )

Washukiwa wa al-Shabaab wamewauwa walimu watatu Ijumaa katika shambulio lililotokea eneo la Qarsa, Kaunti ya Wajir nchini Kenya.

Kamanda wa jeshi la polisi Stephen Ngetich amethibisha alfajiri ya leo shambulizi hilo ambapo mwalimu mmoja alijeruhiwa vibaya sana.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari inaelekea kuwa wanamgambo wa al Shabaab wamehama kutoka upande wa Mandera na kuweka kambi yao Wajir ambapo wameendelea kufanya mashambulizi mara kwa mara katika miezi ya hivi karibuni.

Februari 12, polisi waliokota miili mitatu inayosadikiwa kuwa ya wapiganaji wa al-Shabaab waliouwawa mapema katika operesheni ya polisi kuzuia shambulizi la magaidi hao katika kambi ya polisi huko Kutulo.

Baadhi ya wapiganaji hao wa al-Shabaab walijaribu kushambulia kambi hiyo usiku, lakini walitimuliwa na kukimbilia katika msitu uliokaribu.

Ngetich amesema kuwa askari wa doria baadae walikuta miili mitatu ya washambuliaji hao katika msitu ulioko mpakani baina ya Kenya na Somalia.

Washambuliaji hao wamekuwa wakilenga kuharibu minara ya mawasiliano katika Kaunti ya Wajir.

Sio chini ya minara mitano imeharibiwa katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja. Maafisa wamesema kuwa kupungua kwa mashambulizi ya magaidi huko Mandera ni kutokana na kujengwa kwa ukuta katika mpaka wa nchi hiyo.

Ukuta huo ambao tayari umejengwa kwa kiasi cha kilomita 10 na mpango unaendelea kuongeza eneo la ujenzi wa ukuta huo kufikia kilomita 28.

XS
SM
MD
LG