Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:32

UN, AU yalaani mashambulizi yaliyoua wahamiaji 40 Libya


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat

Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa umelaani mashambulizi ya angani yalifanyika katika vituo vinavyohifadhi wahamiaji nchini Libya na kuua watu 40.

Maafisa wa afya wa Libya wamesema Jumatano kwamba watu hao wote waliouawa na mashambulizi hayo ya anga siku ya Jumanne na wengine 80 kujeruhiwa.

Vyanzo vya habari vimeeleza kuwa mwenyekiti wa Halmashauri ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, ametaka uchunguzi huru ufanyike na hatua zichukuliwe dhidi ya waliohusika na uhalifu huo wa kusikitisha.

Mashambulizi hayo yanamnyoshea kidole Jenerali Khalifa Haftar, anayeendesha uasi nchini Libya. Amekuwa akijaribu kwa miezi mitatu kuukamata mji mkuu Tripoli.

Msemaji wa huduma za dharura nchini Libya, Osama Ali, amelitaarifu shirika la habari la AFP kwamba hiyo ni tathmini ya awali na huenda ikaongezeka.

Amesema wahamiaji 120 walikuwa wanashikiliwa katika jengo la kuhifadhi ndege ambalo lilishambuliwa.

Mjumbe wa tume ya UN ya wakimbizi, Filippo Grandi amesema baada ya mashambulizi hayo kwamba raia hawapaswi kulengwa, na haipaswi kuwashikilia wahamiaji na wakimbizi.

Ameongeza kusema kwamba Libya si sehemu salama kuwarudisha wahamiaji ambao wameokolewa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean kwa njia ya hatari ili kwenda Ulaya.

Grandi ametoa mwito kwa mataifa yote yenye ushawishi kwa pande zote zenye mgogoro kwa pamoja kushirikiana kumaliza mapigano.

XS
SM
MD
LG