Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:37

Waziri Mkuu wa Libya na mpinzani wake bado ni kitendawili


Waziri Mkuu wa Libya,Fayez al-Sarraj
Waziri Mkuu wa Libya,Fayez al-Sarraj

Waziri Mkuu Al-Sarraj alisema mpinzani wake anajaribu kupanga mapinduzi kuiangusha serikali halali na kuchukua madaraka ambapo uharibifu wa utaratibu wa kisiasa ulifanywa na mpinzani Jenerali Khalifa Hafta na sio serikali ya mkataba wa kitaifa

Waziri Mkuu wa Libya, Fayez al-Sarraj alisema mpinzani wake wa madaraka Jenerali Khalifa Haftar anajaribu kupanga mapinduzi na kuichukua Libya kwa lazima. Al-Sarraj alikiambia kituo cha televisheni cha France 24 mjini Paris siku ya Jumatano kwamba Haftar anaota kuingia Tripoli.

Al-Sarraj alisema “shambulizi hili lazima likemewe kwa sababu ni jaribio la kuiangusha serikali halali na kuchukua madaraka, uharibifu wa utaratibu wa kisiasa ulifanywa na Khalifa Hafta, sio serikali ya mkataba wa kitaifa na tupo tayari kurudi kwenye utaratibu wa kisiasa mara masharti yakifikiwa”.

Jenerali Khalifa Haftar
Jenerali Khalifa Haftar

Jenerali Hafta anaongoza serikali hasimu huko mashariki mwa Libya. Jeshi lake la Libyan National Army lilisonga mbele dhidi ya serikali ya Al-Sarraj iliyowekwa na Umoja wa Mataifa mwezi uliopita lakini imekuwa ikikwamishwa na vikosi vya serikali na washirika wao katika viunga vya kusini mwa Tripoli vikishindwa kuchukua mji mkuu.

Baadhi ya raia wa Libya waliokwama katika mapigano walisema hawajali nani anashinda, wanachotaka kuona mapigano yanaisha.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa walisema mapigano yameua watu 440 na kuwalazimisha maelfu kukimbia nyumba zao. Mashambulizi ya anga yanaripotiwa kupiga kituo kimoja huko mashariki mwa Tripoli siku ya Jumanne na kuwajeruhi watu wawili.

XS
SM
MD
LG