Kiongozi huyo alisema hayo alipokutana na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel walipokuwa wanazindua chuo kikuu kipya cha pamoja kati ya Uturuki na Ujerumani mjini Istanbul.
Erdogan ameeleza wasiwasi wake kuhusiana na mzozo wa Libya walipozungumza na waandishi wa habari.
"Ikiwa utulivu hautapatikana kwa haraka iwezekanavyo, hali ya ghasia itakayoongezeka Libya itaathiri kanda zima la Mediterranean," amesema.
Amefafanua : "Tunahitaji kuharakisha juhudi za kutanzua mzozo huo ikiwa hatutaki kushuhudia makundi ya kigaidi ya ISIS na al Qaida kufufuka tena katika nchi hiyo."
Rais Erdogan amesema anamatumiani kwamba jumuiya ya kimataifa haitofanya makosa iliyoyafanya nchini Syria.
Mataifa makuu ya duniani yameimarisha juhudi mnamo wiki chache zilizopita za kutafuta suluhisho la kisiasa kumaliza mzozo wa miaka kadhaa nchini Libya, tangu kuuliwa kwa kiongozi wa muda mrefu Muammar Ghadafi.
Merkel ameeleza kufunguliwa kwa chuo kikuu cha pamoja kuwa ni mfano wa ushirikiano wa kipekee kati ya Uturuki na Ujerumani.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.