Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:44

Uturuki na Rashia zafanikiwa kusitisha mapigano Libya na Syria


FILE - Moshi unaonekana baada ya shambulio la anga kwenye mji wa Sirte, Libya, Sept. 28, 2016.
FILE - Moshi unaonekana baada ya shambulio la anga kwenye mji wa Sirte, Libya, Sept. 28, 2016.

Wananchi wa Tripoli, mji mkuu wa Libya wanasherekea tangazo la kiongozi wa Jeshi la Taifa la Libya, la LNA, Jenerali aliyeasi Khalifa Haftar kwamba, anasitisha mapigano magharibi ya nchi yao kuanzia Jumapili Januari 12.

Tangazo hilo linafuatia makubaliano yaliyofikiwsa kati ya rais Tayyep Erdogan wa Uturuki na mwenzake wa Rashia Vladimir Putin mjini Ankara siku ya Jumatano.

Viongozi hao ambao kila mmoja anaunga upande mwengine wa ugomvi walikubaliana pia kusitisha mapigano nchini Syria, na kutoa wito kwa pande zote zinazogombana kuanza mazungumzo katika nchi zote mbili.

Awali Haftar alipinga makubaliano hayo ya kusitisha mapigano lakini alibadili msimamo wake hapo Jumamosi.

FILE PHOTO: Khalifa Haftar, kiongozi wa kijeshi wa Libya anaeshikilia eneo la mashariki ya nchi. May 29, 2018. REUTERS
FILE PHOTO: Khalifa Haftar, kiongozi wa kijeshi wa Libya anaeshikilia eneo la mashariki ya nchi. May 29, 2018. REUTERS

Msemaji wa LNA Ahmed Mismari alitangaza uwamuzi huo kwa masharti kwamba upandewapili unaheshimu mkataba huo.

Ahmed Mismari, msemaji wa Jeshi la Taifa la Libya LNA

Uwongozi wa Jeshi la Taifa la Libya unatangaza usitishaji mashambulizi magharibi ya nchi kuanzia usiku wa manane wa Januari 12 2020, kwa sharti kwamba upandewa pili unatekeleza usitishaji mapigano kwa wakati huo huo. Ukiukaji wowote wamakubaliano haya yatajibiwa vikali.

Siku ya Jumapili Rais Erdogan amekua na mazungumzo mjini na Fayez al-Sarraj, waziri mkuu wa serikali inayoitambuliwa na Umoja wa Mataifa ambayo anaiunga mkono.

Jeshi linalongozwa na haftar ambalo lilianza mashambulizi makali ya kuuteka mji mkuu wa Tripoli hapo April 4 inasaidiwa na Rashia, Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Huko Syria nako usitishaji mapigano unatarajiwa kuanza kutekelezwa Jumapili, ingawa shirika la kutetea haki za binadam la Syrian Observatory for Human Rights, linalofuatia vita huko Syria linaripoti kwamba watu 17 waliuliwa Juammosi na wengine 40 kujeruhiwa baada ya jeshi la anga la Syria kushambulia miji minne katika jimbo la kaskazini magharibi la Idlib.

Haijajulikana bado ikiwa serikali ya Damuscus inayoungwa mkono na Rashia na Iran itaheshimu makubaliano hayo.

Vladimir Putin akutana na Bashir al Asaad mjini Damuscus Januari 7, 2020
Vladimir Putin akutana na Bashir al Asaad mjini Damuscus Januari 7, 2020

Harakati za kusitisha mapigano Libya na Syria zimekuwa zikifanyika wiki nzima kati ya nchi za Ulaya na Mashariki ya kati ambapo viongozi wa mataifa mbali mbali wamekuwa wakikutana na pande zinazo zozana katika nchi hizo mbili.

Siku ya Ijuma Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alitangaza kutakuwepo na mkutano wa amani wa Libya mjini Berlin hivi karibuni baada ya kukutana na Rais Vladimir Putin mjini Moscow.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha siku ya Ijuma kuongeza muda wa kupeleka msaada wa dharura nchini Syria, ikiwa pia kuelekea jimbo la upinzani la Idlib.

XS
SM
MD
LG