Sekta ya Teknolojia, benki, viwanda vya nguo na burudani zimetuma ujumbe kuunga mkono wale wanaoandamana dhidi ya vitendo vya polisi dhidi ya watu weusi.
“Nimestushwa na idadi ya watendaji wakuu ambao wamejitokeza kuongelea hilo kwa mara ya kwanza,” amesema Kellie McElhaney, Mhadhiri katika Chuo cha Biashara cha Haas huko UC Berkeley na muasisi wa Kituo cha Uwiano, Jinsia na Uongozi katika chuo hicho.
Nini kinachopelekea biashara kupaza sauti, amesema mhadhiri huyo, ni ukatili ulionekana katika picha ya video ukionyesha afisa polisi huko Minneapolis akimwekea goti nyuma ya shingo ya George Floyd, ambaye alikufa.
Makampuni hayo “yanaendeshwa na binadamu,” amesema mhadhiri huyo. “Wana wafanyakazi, watendaji, wateja weusi na rangi nyingine. Kuna kubahatisha kwa hali ya juu lakini faida ya kukosoa vitendo vya polisi vinazidi hatari nyingine.”
Netflix, Google na Citibank
Kampuni ya Netflix ilituma ujumbe wa tweet “kukaa kimya ni kuunga mkono uhalifu,” ikiongeza kuwa “tuna wajibu kwa washiriki, wafanyakazi, watengenezaji na vipaji wetu Weusi kupaza sauti.
Kampuni ya Google iliongeza katika ukurusa wake wa kutafiti : “Tunasimama pamoja kuunga mkono usawa wa rangi, na wote wale wanaotafuta hilo.”
Twitter imebadilisha akaunti yake na ina ujumbe #BlackLivesMatter (MaishaYaWatuWeusiMuhimu).
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Microsoft Satya Nadella amewaambia wafanyakazi “ kuungana nami na kila moja katika uongozi wa juu, katika kushinikiza kupatikana mabadiliko ndani ya kampuni, katika jumuiya zetu na jamii kwa ujumla.”
“Ubaguzi unaendelea kuwepo katika kiini cha maumivu makali na sura mbaya kwa jamii yetu,” Afisa wa Fedha Mkuu wa Benki ya Citibank Mark Mason, ambaye ni Mmarekani mweusi, ameandika katika blogi yake. “Muda wa kuwa hilo ni kweli, maadili pacha ya Marekani ambayo ni uhuru na usawa hayawezi kufikiwa.”
Biashara za rejareja kama vile Maduka ya Target, ambalo liliharibiwa na kuibiwa katika mji mbalimbali nchini, wao pia wamepaza sauti zao. Kifo cha mtu mweusi aliyekuwa ameshikiliwa na polisi mzungu ndio iliyoibua “hasira iliyojificha kwa miaka mingi,” amesema Afisa Mtendaji Mkuu wa Target, yenye makao yake makuu Minneapolis.