Waandamanaji walikusanyika wakati wa chakula cha mchana katika kituo cha biashara klichopo katika eneo lenye harakati katikati ya wilaya ya kibiashara.
Mwandamanaji Jerome Lau mwenye umri wa miaka 70, amesema :“Kuchukua pumzi yangu ya mwisho, nitajitokeza na kupambana kwa ajili ya uhuru wangu. Hakuna uhuru wa kujieleza, kukusanyika na elimu. Wanajaribu kukandamiza uhuru huo kwa kadiri wanavyoweza.”
Waandamanaji wakiheshimu amri ya kutokaribiana kuepusha maambukizi ya virusi vya corona walikuwa wamebeba mabango yaliyoandikwa “Iwacheni Huru Hong Kong – Mapinduzi hivi sasa.”
Mabango mengine yaliyotundikwa katika roshani kwenye magorofa ziliandikwa “ Ikomboeni Hong Kong, Mapinduzi ya Nyakati Zetu” na “Uhuru wa Hong Kong,” kile hasa ambacho waandamanaji wanapigania na nini Beijing wanajaribu kukandamiza.
Wakati huo huo Polisi walikuwa wamesimama pembeni nje ya kituo cha biashara lakini hawakuonekana kutaka kuingilia kati.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo na Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi wamepinga sheria mpya ya usalama ya China inayoshinikizwa Hong Kong.
Kauli nzito za kulaani sheria hiyo imetolewa Ijumaa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Maas, aliyesema Umoja wa Ulaya (EU) unakubaliana kuwa Hong Kong “kiwango chake cha juu cha uhuru wake haiwezekani kuachiwa kukandamizwa.”
“Tunatarajia kuwa uhuru na haki za raia zitaheshimiwa na kwa kanuni za nchi mmoja, mifumo miwili,” Maas amesema.