Kipimo cha hisa cha Japan, Nikkei kilifunga biashara yake kikiwa juu kwa asilimia 0.2, wakati kile cha Taipei TSEC kilihitimisha mauzo yake kikiwa juu kwa asilimia 0.6. Vipimo vya biashara Hong Kong, Shanghai na Sydney vilikuwa viko kwenye wigo la mauzo hasi.
Wawekezaji katika nchi hizi kwa namna fulani wanaonekana hawakuvutiwa na tangazo la Beijing, kuwa kiwango cha bidhaa zake zinazosafirisha nje kimeongezeka kwa asilimia 3.5 kuliko mwaka jana, ikiwa ni dalili nyingine kuwa uchumi wa dunia unafufuka kutokana na janga la virusi vya corona.
Wakati huo huo biashara kwenye masoko ya Ulaya ilikuwa inaendelea kupanda, wakati kipimo cha hisa cha London FTSE kikiwa juu kwa asilimia 0.4 hadi asubuhi, nacho cha Paris CAC-40 kilipanda kwa asilimia 0.5 na kile cha, Frankfurt DAX kikiwa juu kwa asilimia 0.7.
Aidha, bei kwenye masoko ya mafuta zilikuwa zikiendelea kupanda Alhamisi, wakati bei ya kampuni ya West Texas Intermediate, ambayo ni kipimo cha soko la Marekani la mafuta ghafi pipa moja ikiuzwa kwa dola za Marekani 29.08, ikiwa imepanda kwa asilimia 0.3. Nayo bei ya kipimo cha kimataifa cha Brent haikubadilika ikiwa pale pale, yani dola 29.73 kwa pipa.
Na katika vipimo vya biashara vya hisa za Marekani, Dow Jones, S&P 500 na Nasdaq hali haikuwa mbaya kutokana na bishara kuwa juu kwa asilimia 1.