Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 15:14

Hofu ya kudorora uchumi wa dunia yaangusha thamani ya hisa


Wafanyabiashara wakiwa wanafanya manunuzi na kuuza hisa katika ukumbi wa Soko la Hisa la New York, Agosti 12, 2019. REUTERS/Eduardo Munoz
Wafanyabiashara wakiwa wanafanya manunuzi na kuuza hisa katika ukumbi wa Soko la Hisa la New York, Agosti 12, 2019. REUTERS/Eduardo Munoz

Thamani ya hisa katika masoko ya Ulaya na Marekani ilishuka sana Jumatano, huku ishara muhimu ya kipimo cha uchumi ikionyesha kuna uwezekano wa kudorora kwa uchumi wa dunia hapo mwakani.

Kushuka kwa hisa

Wachambuzi wanasema hii inatokana na ripoti za kushuka kwa kukua kwa uchumi wa Ujerumani na China pamoja na vita vya biashara kati ya China na Marekani.

Thamani za hisa muhimu katika soko la Wall Street New York zilishuka kwa asilimia 2 huku thamani ya hisa za ulaya zikiporomoka kwa kiwango karibu sawa.

Rais Trump

Hisa za Dow Jones moja wapo ya hisa kuu 30 za Marekani ilishuka kwa pointi 600 baada ya kupanda ghafla Jumanne pale Rais Donald Trump kutangaza kwamba anachelewesha kuweka ushuru mpya wa asili mia 10 kwa bidhaa za china zinaoingia marekani.

Alisema kuwa tunafanya hivyo kwa ajili ya kipindi cha Krismasi endapo tu baadhi ya bidhaa zitakazowekewa ushuru zitakuwa na athari kwa wateja wa Marekani.

Wachambuzi wanasema takwimu za kuanza kudororo kwa uchumi wa ujerumani na kupunguka ukuwaji wa uchumi wa China kufikia asili mia 5 mwezi Julai ikiwa chini zaidi kuliko ilivyotazamiwa.

Na kutokana pia na vita vya kibiashara na Marekani na takwimu hizo ni ishara ya uwezekano wa kudorora kwa uchumi wa dunia. Robert Halver mkuu wa uchambuzi wa masoko katika benki ya Baadaer Ujerumani anasema kushuka kwa uchumi wa ujerumani katika robo ya pili ya mwaka huu ilikuwa inatarajiwa.

Robert Halver Mkuu wa uchaguzi wa masoko

Lakini cha muhimu tunabidi kufanya kitu kuleta mabadiliko. Ujerumani taifa kuu la usafirishaji bidhaa nje ulaya linakabiliwa na changamoto na sisi hatuleti mapendekezo mepya ya mageuzi ya sera miundombinu ili tunedelea kuwa washindani kwa kipindi cha muda mrefu.

Hali hiyo yote ilimsababisha mwenyekiti wa benki kuu ya Marekani Jerrome Powell kutangaza Jumatano kwamba wameamuwa kupunguza kiwango cha riba kwa asili mia robo kutoika asili mia 2 na robo hadi asili mia 2.

Jerome Powell,

Mwenyelkiti wa Benki Kuu, Marekani amesema Lengo ni kuhakikisha "tunajilinda dhidi ya hatari za kushuka uchumi kutokana na ukuwaji dhaifu wa uchumi wa duniana wasi wasi katika sera za biashara."

Wachambuzi wanasema kutokana na kujitokeza ishara za kushuka kwa uchumi kutalazimisha mabenki kuu mengine ya dunia kupunguza viwango vyao vya riba.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC

XS
SM
MD
LG