Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:12

Trump aidhinisha mchakato wa kuitoza China ushuru zaidi kwa bidhaa zilizosalia


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais Donald Trump wa Marekani, amewaagiza maafisa wake kuanza mchakato wa kuongeza ushuru kwa bidhaa zote kwa jumla zilizobakia zinazoingia kutoka China zinazokadiriwa kuwa na thamani ya dola za Marekani bilioni 300.

Mwakilishi wa Marekani katika mambo ya biashara Robert Lighthizer ametoa tangazo hilo katika tamko lake Ijumaa baada ya Marekani kuongeza ushuru kutoka asilimia 10 hadi 25 kwa bidhaa zinazoagizwa nchini Marekani kutoka China zenye thamani ya dola bilioni 200.

Ameeleza kuwa maelezo kamili juu ya mchakato huo katika kipindi cha kuchukua maoni ya wananchi juu ya pendekezo la ongezeko la ushuru yatachapishwa muda sio mrefu.

Hali hii imetokea baada ya Marekani na China kumaliza mazungumzo yao ya kibiashara hivi karibuni bila ya kutangaza makubaliano yoyote.

Trump alituma ujumbe wa Tweeter juu yauamuzi huo Ijumaa jambo ambalo wachambuzi wa masuala ya kibiashara wanasema uamuzi huo utazidi kongeza mvutano wa kibiashara baina ya Marekani na China.

China inashikilia nafasi ya pili kwa kuwa na uchumi mkubwa duniani. Adhabu hiyo imetolewa baada ya Rais Trump kusema ushuru huo utaifanya China kubadilisha mwenendo wake wa kufanya biashara, utoaji wake ruzuku na kuheshimu haki miliki katika biashara.

Trump amewaambia waandishi kuwa anaamini "ushuru kwa ajili ya nchi yetu ni wenye nguvu," na utanufaisha uchumi wa Marekani.

Baadhi ya wachumi, wanatabiri kuwa ushuru kama huu utapunguza kukua wa uchumi wa Marekani

David French wa Jumuiya ya Biashara za Rejareja ya Marekani amesema katika mahojiano na VOA " mkakati wa mazungumzo unaojikita kwenye ushuru sio njia sahihi, na kueleza matumaini kuwa China "itajikusuru kadiri itavyoweza kufikia maridhiano ili kuepusha janga hili la kibiashara."

Nayo China imesema mazungumzo kati yake na Marekani yataendelea ili kutafuta ufumbuzi juu ya mgogoro huo.

XS
SM
MD
LG