Hii ni mara ya tatu Kenyatta kukutana na Xi Jinping katika kipindi cha mwaka mmoja, ambapo Xi Jinping amesema mkutano huo ni muhimu kwa ajili ya kuboresha uhusiano mwema kati ya Kenya na China.
Xi Jinping, amesema anafurahishwa na jinsi Kenyatta alivyo na msimamo thabithi dhidi ya shutuma zinazotolewa kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, na ushirikiano wa China na Afrika.
Viongozi hao wamekubaliana kuimarisha uhusiano wao katika kufanikisha miradi mbalimbali.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington DC.