Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 09:56

China, EU kuimarisha ushirikiano


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa China Xi Jinping
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa China Xi Jinping

Rais wa China Xi Jinping ametoa wito wa kuendeleza uhusiano muhimu kati ya nchi yake na Ufaransa na kuimarisha ushirikiano wao chini ya misingi thabiti wa kuheshimiana, mara alipomaliza ziara ya siku tatu nchini Ufaransa siku ya Jumatano.

Akiwa huko Ufaransa alikutana mara kadhaa na mwenyeji wake Emmanuel Macron na kusaini mikataba kadhaa ya biashara na ushirikiano wa kiuchumi, elimu na utamaduni.

Mkutano wa pamoja

Miongoni mwa waliohudhuria mazungumzo ni pamoja na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Jean Claude Juncker.

Wawili hao walialikwa na mwenyeji wao Rais Macon aliyetaka kusisitiza nia yake ya kuona nchi za Ulaya zinachukua msimamo wa pamoja katika kushirikiana na China.

Hatua hii ni kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa, baada ya Rais Donald Trump kuiondosha Marekani katika mikataba kadhaa ya kimataifa.

Emmanuel Macron

Emmanuel Macron, Rais wa Ufaransa amesema : "Sote tuna mambo tunayotofautian, hilo likiwa ni jambo la kawaida la kibinadamu. Lakini sisi tunaiheshimu Uchina na tunadhamira ya kuwa na majadiliano na ushirikiano nayo, na bila ya shaka tunatarajia mshirika wetu mkuu (China) ataheshimu umoja uliyopo ndani ya Umoja wa Ulaya.

Viongozi wa Ulaya na china wamesisitiza juu ya haja ya kutanzua tofauti kati yao na kuahidi kufanya kazi kwa pamoja katika masuala yenye maslahi ya pamoja.

Rais Xi amesisitiza juu ya haja ya kupunguza mvutano kati ya nchi yake na Umoja wa Ulaya katika masuala kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, biashara na kutoaminiana.

Rais Xi Jinping alitembelea Ufaransa na Italy kwa lengo la kuyataka mataifa ya Ulaya kujiunga na mradi wake mkubwa wa miundo mbinu, unaohusisha mataifa 71 hivi sasa unaofahamika kama One Belt and One road, na kutayarisha mkutano wa viongozi kati ya China na Umoja wa Ulaya mjini Brussels hapo April 9.

Kiongozi wa Uchina alikiri kuwepo kwa tofauti hizo na mashindano lakini amesema kuna haja ya kuimarisha ushindani mzuri na ushirikiano wenye manufaa kwa wote.

Xi Jinping

Rais wa China Xi Jinping amesema : "Tunasonga mbele bega kwa bega tuna shirikiana kwa wema na mabaya. Hatuwezi kuruhusu dhana kati yetu kuharibu wema wetu."

Angela Merkel

Kiongozi wa Ujerumani alieleza kwamba Umoja wa Ulaya unataka kushiriki katika mradi wa One Belt one Road lakini wanataka kushirikiana kwa kugawanya pamoja majukumu.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema : "Ninaamini ni mradi muhimu sana. Sisi kama nchi za ulaya tunataka kuwa na jukumu kubwa katika mradi na ni lazima kuwepo aina ya kugawanya majukumu kwa pamoja."

Italy inakuwa nchi ya kwanza ya Ulaya kujiunga na mradi huo na akiwa katika ziara hiyo ya ulaya Xi alitia saini mikataba kadhaa ya biashara na Itali na Ufaransa na kuahidi kununua ndege 290 za Airbus ya Ulaya aina ya A320.

Pia ameahidi kuwa atasaini mikataba kadha yenye thamani ya jumla ya dola za Marekani bilioni 45 na Ufaransa.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC

XS
SM
MD
LG