Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:50

Marekani na China wanakutana kujadili ushuru wa bidhaa za China


Timu ya wawakilishi wa biashara Marekani na China wanakutana wiki hii Washington
Timu ya wawakilishi wa biashara Marekani na China wanakutana wiki hii Washington

Matamshi ya Trump kwenye Twitter kuhusu kuweka ushuru mpya kwa China yalipelekea masoko ya Asia na Marekani kuwa na wakati mgumu Jumatatu na iliongeza khofu juu ya idadi ya mashauriano ya biashara kati ya nchi hizo mbili

China inaeleza kwamba wapatanishi wake wanajiandaa kusafiri kuelekea Marekani kwa duru nyingine ya mazungumzo ya biashara wiki hii hata baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutishia kuongeza ushuru kwa bidhaa za China zenye thamani ya mabilioni ya dola baada ya kulalamikia kwamba utaratibu wa majadiliano unachukua muda mrefu.

Matamshi ya Rais Trump kwenye Twitter siku ya Jumapili kuhusu kuweka ushuru mpya kwa China yalipelekea masoko ya Asia na Marekani kuwa na wakati mgumu siku ya Jumatatu na iliongeza khofu juu ya idadi ya mashauriano ya biashara kati ya Marekani na China. Licha ya soko kushuka vyombo rasmi vya habari China vilikuwa kimya juu ya matamshi ya Trump.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje China, Geng Shuang
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje China, Geng Shuang

Saa kadhaa baadae msemaji wa wizara ya mambo ya nje nchini China, Geng Shuang aliwaambia waandishi wa habari kwamba China inajaribu kupata taarifa zaidi kuhusu matamshi ya Trump kuhusiana na ushuru mpya lakini alieleza kwamba timu ya mashauriano ya Beijing bado inajiandaa kusafiri kwenda nchini Marekani kwa mazungumzo hayo wiki hii.

XS
SM
MD
LG