Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 14:27

Canada inatafuta taarifa za raia wake mwingine aliyekamatwa China


Justin Trudeau, Waziri Mkuu wa Canada
Justin Trudeau, Waziri Mkuu wa Canada

Justin Trudeau alisema haamini kwamba raia wa tatu wa Canada aliyekamatwa China ana uhusiano wowote na kesi nyingine akieleza kwamba hiyo ni kesi tofauti.

Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau alisema serikali yake inajaribu kupata taarifa zaidi kuhusu raia wa tatu wa Canada aliyekamatwa nchini China. Watu wawili wengine walikamatwa muda mfupi baada ya polisi wa Canada kumkamata mtendaji wa juu wa kampuni ya teknolojia ya China kwa waranti ya Marekani ya Disemba mosi.

Meng Wanzhou
Meng Wanzhou

Meng Wanzhou anashutumiwa kwa kukiuka vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran. Trudeau alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatano haamini kwamba raia wa tatu wa Canada aliyekamatwa ana uhusiano wowote na kesi nyingine akieleza kwamba hiyo ni kesi tofauti.

Alipoulizwa kwa nini serikali yake inaonekana kutofanya vya kutosha kuhakikisha raia hao wa Canada wanaachiwa huru alieleza ”wa-canada wanafahamu kwamba ingawaje msimamo wa kisiasa huenda ukawa wa kuridhisha tu katika kipindi cha muda mfupi na kuhisi kama vile unapiga kelele na unafanya jambo muhimu, huenda isichangie moja kwa moja kupata matokeo tunayotaka".

Japokuwa maafisa wa Canada hawajahusisha moja kwa moja uhusiano wa kuwekwa kizuizini watu hao huko China na kukamatwa kwa Meng balozi wa zamani wa Canada kwa China, David Mulroney anaeleza hilo linawezekana.

XS
SM
MD
LG