Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:35

Mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani yaingia siku ya pili


Naibu Waziri Mkuu wa China, Liu He akiwa na Waziri wa Fedha Steven Mnuchin nje ya ofisi za Mwakilishi wa Biashara wa Marekani Washington, Marekani Mei 9, 2019.
Naibu Waziri Mkuu wa China, Liu He akiwa na Waziri wa Fedha Steven Mnuchin nje ya ofisi za Mwakilishi wa Biashara wa Marekani Washington, Marekani Mei 9, 2019.

Wajumbe katika mazungumzo ya kibiashara kati ya Marekani na China wanakutana kuendelea na mazungumzo kwa siku ya pili, Ijumaa, masaa machache baada ya ushuru wa Marekani dhidi ya bidhaa za China kuanza kutumika.

Marekani imeongeza ushuru kwa bidhaa zinazoletwa kutoka China kati ya asilimia 10 hadi 25 ambazo zina thamani ya dola za Marekani bilioni 200 kutoka China, huku Naibu Waziri Mkuu wa China Liu He, na waakilishi wa Marekani wakianza mazungumzo kutafuta makubaliano.

Liu He, anaongoza ujumbe wa China katika mazungumzo hayo yanayokabiliwa na vitisho vya kutofanyika baada ya utawala wa Trump kuishutumu Beijing kwa kuchukua hatua zinazorudisha nyuma yale yaliyokuwa yamefikiwa kati ya nchi hizo mbili hadi sasa.

Utawala wa Trump una matumaini kwamba ushuru mpya utailazimisha China kubadilisha sera zake za kibiashara na hati miliki.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC


XS
SM
MD
LG