Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:26

Silicon Valley na athari ya maamuzi ya Trump


Silicon Valley, California
Silicon Valley, California

Wanaziita ni athari za utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump. Hii ni kutokana na kuongezeka uchunguzi unaofanywa na serikali yake katika vitega uchumi vya China huko Silicon Valley.

Silicon Valley, ambayo ni makao makuu ya teknolojia Marekani, wanasema inamaanisha kuwa baadhi ya makubaliano yaliyofikiwa hayataweza kutekelezwa. Baadhi yake hayatoweza hata kuzungumziwa.

Kwa kawaida biashara zinazoanzishwa zinatafuta fedha na kuvutiwa na fursa zilizoko katika soko la China, lakini hali ilivyo hivi sasa haziendelezi uwekezaji China, wameeleza.

Baada ya miaka kadhaa ya kukua kwa ushirikiano kati ya China na Silicon Valley, ambayo ni makao makuu ya teknolojia ya Marekani yenye makao yake makuu huko jijini San Francisco, kaskazini mwa jimbo la California, imejikuta imekwama kutokana na mvutano uliyopo kati ya Beijing na Washington.

Silicon Valley wamebaki kujiuliza ni nchi gani itashinda katika ushindani huo kuweza kutengeneza kizazi kijacho cha mawasiliano ya teknolojia ya kisasa.

“Juhudi za ubunifu wa China ni mpana na wa kina,” amesema Michael Wessel, kamishna wa Tume ya kuhakiki hali ya Uchumi na Usalama kati ya Marekani na China, katika mahojiano yake na bunge la Marekani.

“China inataka kuwa kiongozi katika ubunifu wa kimataifa na inafanya kila liwezekanalo kisheria na kinyume cha sheria kufikia malengo yake," amesema.

XS
SM
MD
LG