Rais-mteule Donald Trump amekutana Jumatano na viongozi wa makampuni ya teknohama ya Marekani, wengi kati yao walikuwa wapinzani wake wakuu wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka huu, lakini hakukuwa na dalili zozote za kubaki hali ya uhasimu huo wakati wa mkutano wao.
Ofisi ya Trump imeeleza kwamba anataka kuanza “mazungumzo na ushirikiano” ili kuchochea ubunifu na kutengeneza ajira zaidi.
Mkutano huo ulofanyika katika makao makuu ya Trump huko New York umehudhuriwa pamoja na mkuu wa utendaji wa Facebook Sheryl Sandberg, mkuu wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos, mkuu wa kampuni yaTesla, Elson Musk na muasisi shirika wa kampuni ya Google Larry Page.
Trump alianza mkutano kwa sauti ya ukirafiki na maridhiano.
“Hakuna mtu anayefikia sifa za hawa watu waliopo katika chumba hiki. … Tunawataka mwendelee na hizi hatua za ubunifu,” Trump alisema. “Kitu chochote tunachoweza kufanya kusaidia hili lisonge mbele tutafanya ili kushirikiana na nyinyi.”
Trump aliwapa fursa viongozi hawo kuwasiliana nae moja kwa moja kama wanataka kuongea na yeye, na akapendekeza wakutane tena, mara kwa mara kila baada ya miezi mitatu.
Ofisi ya rais mteule imesema Trump alikuwa “ tayari kuwasikiliza” katika mazungumzo hayo, na kuwa muelekeo alochukua “ulipokelewa vizuri” na viongozi hao.
Baada ya mkutano hakuna kiongozi yoyote aliyezungumza na waandishi, lakini baadae Bezos alitoa tamko rasmi akieleza kuwa mazungumzo yao “yalikuwa yana tija.”
“Nilitoa maoni kwamba ni muhimu kwa serikali kufanya ubunifu kuwa moja kati ya misingi yake mikuu katika utawala wake, kitu ambacho kitatengeneza ajira nyingi kote nchini, katika secta zote, sio tu katika teknolojia- kilimo, miundombinu na viwanda- lakini sehemu zote,” alisema.
Viongozi wengi katika jumuiya ya teknolojia walikuwa na manung’uniko yaoTrump kuwa rais kabla ya uchaguzi kwa sababu ya msimamo wake mikali dhidi ya China, vitisho vyake vya kusitisha mikataba ya kibiashara na mpango wake wa kuzuia uhamiaji, jambo ambalo litawazuia wafanyakazi wenye ujuzi mkubwa ambao wako tayari kujiunga na kampuni za teknolojia kuja Marekani.
.Barua ya wazi iliyo sainiwa Jumanne na wafanyakazi zaidi ya 200 kutoka makampuni ya teknolojia iliapa kutomsaidia Trump kutengeneza daftari ya takwimu itayo fuatilia watu kwa misingi ya dini zao, au kufanya uwezekano wa kuondolewa nchini.
Wakati wa kampeni, Trump mara nyingi alihitilafiana na waatalamu hao kutoka eneo linalofahamika kama Silicon Valley. Aliwataka wapiga kura kususia kampuni ya Apple kwa sababu ya msimamo wake kuhusu kuweka siri na kuapa “kuilazimisha Apple kuanza kutengeneza computer na iphones Marekani.”
Alimshabulia mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg kuhusiana na suala la uhamiaji na kumshutumu Bezos kwa kutumia gazeti analomiliki, The Washington Post, katika mbinu ya kukwepa kodi. Gazeti hili maarufu la kila siku limekuwa likimkosoa Trump katika kurasa zake za maoni.
Lakini Trump amewaahidi viongozi wa kampuni hizi za teknolojia ataweka pamoja “mikataba ya biashara yenye uadilifu” ambayo itafanya wepesi kwenu (makampuni) kufanya biashara katika nchi jirani.”
Kabla ya kuingia katika mkutano, Kiongozi wa Oracle Safra Catz alisema kwamba kama Trump “atafanya marekebisho ya kodi”, atapunguza masharti na kufanya mazungumzo juu ya mikataba bora ya biashara, jumuiya ya wanateknolojia itakuwa na nguvu na uwezo wa ushindi kuliko zama zozote.
Wakati huo huo Rais-mteule wa Marekani Donald Trump amemteua hasimu wake wa kisiasa ambae ni Gavana wa zamani wa Texas, Rick Perry, kuongoza Wizara ya Nishati, ikiwa ni idara kubwa Perry aloitaka iondolewe kwani ilikuwa haina faida.
Perry, ambae mara mbili aligombea urais kwa tiketi ya Republican, alimwita Trump “ni saratani ya conservatism” katika hatua za mwanzo uchaguzi wa mrefu wa chama katika kinyanganyiro cha kupendekeza mgombea.
Lakini baada ya kujiengua kutoka katika mchuano kwa kupata kura chache, Perry ambae ni miaka 66 alimuunga mkono Trump, akisema kuwa mfanyabiashara huyo wa New York alikuwa sio chaguo lake la kwanza or la pili katika nafasi ya urais, lakini bado alikiri kuwa “ni chaguo la wananchi.”
Trump siku ya Jumatano alimtaja rasmi Perry kuwa ataingoza idara hiyo ambayo ina wafanyakazi, 100,000, inayosimamia silaha za nuclear za taifa na inaendeleza miradi ya maendeleo inayo lenga nishati salama.
Chama cha Republican chapata mwenyekiti mwanamke
Rais-mteule pia ameteua Ronna Romney Mc Daniel, kiongozi wa chama cha Republican Michigan kuongoza kamati ya taifa ya Republican, akichukua nafasi ya Reince Priebus, ambae atakuwa Chief of staff wa Ikulu ya White House.
Mc Daniel ni mpwa wa aliyekuwa mgombea wa urais wa chama cha Republican Mitt Romney, ambae alikuwa kati ya wale waliokuwa wanafikiriwa kuchukua nafasi ya waziri wa mambo ya nje. Atakuwa ni mwanamke wa kwanza kuchukua nafasi hiyo ya chama katika kipindi cha miaka 40- tangu Mary Louise Smith wa Iowa aliposhikilia nafasi hiyo mwaka 1974.
Wizara ya mambo ya ndani
Trump pia inasemekana atamteua mwakilishi wa Republican katika jimbo la Montana, Ryan Zinke ambae alikua mwanamaji wa kikosi maalum cha Navy Seal kuongoza wizara ya mambo ya ndani.
Zinke, ameelezewa na gazeti la The Washington Post kama ni mwindaji na mvuvi wa muda mrefu, pia ni mshabiki wa kuweka ardhi za taifa chini ya umiliki wa serikali kuu. Msimamo wake huo utamweka katika hali ngumu kwani wale wafuasi wa chama cha Republican wanapendelea sera ya ubinafsishaji, au kuweka ardhi hizo chini ya umiliki wa majimbo.
Trump pia ameweka wazi kwamba hafikirii ni sahihi kwa ardhi za taifa kuwa chini ya udhibiti wa majimbo.