Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:55

Marekani na China wamepiga hatua mazungumzo kuhusu biashara


Waziri wa fedha wa Marekani, Steven Mnuchin na Waziri Mkuu wa China Liu He
Waziri wa fedha wa Marekani, Steven Mnuchin na Waziri Mkuu wa China Liu He

Waziri wa fedha wa Marekani, Steven Mnuchin alisema kwamba wamefanya mafanikio kadhaa na anafikiri wana mkataba uliokamilika kwa asilimia 90. Alisema China ilitaka kurudi nyuma kwenye vitu kadhaa wakati wa mazungumzo yao madai ambayo China inakanusha

Waziri wa fedha wa Marekani, Steven Mnuchin alieleza Jumapili kwamba Rais Donald Trump atakuwa na furaha kuongeza kodi kwa bidhaa zaidi zinazoingia Marekani kutoka China kama hatofikia mkataba wa biashara na Rais wa China, Xi Jinping.

Marais wote wawili wamepangiwa kukutana baadae mwezi huu kwenye mkutano wa kundi la G20 nchini Japan. Mnuchin alikiambia kituo cha televisheni cha CNBC cha Marekani kwamba wamefanya mafanikio kadhaa na anafikiri wana mkataba uliokamilika kwa asilimia 90. Alisema kwamba China ilitaka kurudi nyuma kwenye vitu kadhaa wakati wa mazungumzo madai ambayo China inakanusha.

Steven Mnuchin, waziri wa fedha wa Marekani
Steven Mnuchin, waziri wa fedha wa Marekani

Mnuchin aliendelea kueleza kwamba wamesitisha mashauriano na hatua ijayo inategemea mkutano wa Rais Trump na Xi huko Osaka kwenye mkutano wa viongozi wa mataifa yenye uchumi mkubwa wa G20 hapo Juni 28 hadi 29.

Trump tayari ameshaweka ushuru kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 200 lakini hivi sasa anafikiria kuongeza kodi kwa bidhaa yenye thamani ya dola 325 bilioni. Hiyo itajumuisha takribani kila kitu China inachosafirisha kuelekea Marekani.

Nchi hizi mbili zenye uchumi mkubwa duniani zimekuwa na tofauti kwa miezi kadhaa juu ya mkataba wa biashara lakini hawakuweza kufikia makubaliano.

XS
SM
MD
LG