Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:05

NASA: Biashara ya safari za anga za juu iko njiani


Mwanaanga wa NASA Anne McClain akiwa anajaribu chombo cha anga za juu
Mwanaanga wa NASA Anne McClain akiwa anajaribu chombo cha anga za juu

NASA itafunguwa sehemu ya vituo vyake vya angani vya kimataifa kwa ajili ya fursa zaidi za kibiashara, imetangaza siku ya Ijumaa, ambapo inaruhusu makampuni kutumia vituo vyake vya anga za juu kwa namna mbalimbali, ikiwemo fursa kwa abiria wa kawaida wenye nia ya kufika anga za juu.

NASA ni Shirika linalojitegemea la serikali kuu ya Marekani linalosimamia programu za angani za kiraia na tafiti za sayansi ya safari za anga za juu. NASA ilianzishwa mwaka 1958.

Shirika hilo la safari za anga za juu lilisita kuanza safari za kibiashara siku za nyuma, lakini gharama za kuendesha vituo hivyo vya angani, ambazo ni moja ya gharama za juu kuliko zote za shirika hilo, hivi sasa linaigharimu dola za Marekani bilioni 3 mpaka 4 kwa mwaka au takriban zaidi ya dola milioni 8 kwa siku.

Uongozi wa NASA umeweka wazi kuwa shirika hilo linataka hatimaye kukabidhi uangalizi wa kituo cha angani na maeneo yake ya angani, eneo la chini la sayari ya dunia, kwa sekta binafsi.

Kwa kukabidhi usimamizi wa kituo cha angani kwa kampuni za biashara, NASA inaweza kujipatia pesa zaidi kuendesha shughuli wanazozipendelea zaidi, kama vile kujenga kituo kipya angani karibu na mwezi na kutuma wanadamu katika sayari ya lunar.

Mwisho wa mwaka 2018, shirika hilo lilichaguwa makampuni 12 kutafiti juu ya uwezekano wa kuendeleza uchumi wa anga ya chini ya sayari ya dunia na njia bora ya kuchochea azma na mahitaji ya binadamu kusafiri anga za juu. Inapozungumziwa anga ya chini ya sayari ya dunia ni umbali usiozidi kilomita 2,000 au maili 1,240.

Watafiti hao walijadiliana njia mbalimbali jinsi makampuni hayo yangeweza kutengeneza faida katika kituo cha angani, na washiriki hao waliamua kuwa kuruhusu makampuni kujenga na kunadi bidhaa zao kwa kutumia rasilimali za vituo vya angani kutaweza kusaidia kuchochea uchumi ambao NASA inakusudia kuendeleza.

Lakini watafiti hao wanaeleza kuwa ifahamike kufikia anga za juu kabisa gharama zake sio kidogo.

"Safari za anga za juu kabisa zitafanyika mara mbili kwa mwaka, au tutapeleka wanaanga 12 kwa mwaka, na hilo litagharimu kiwango kikubwa. Gharama za usafiri na malazi zitatozwa na sekta binafsi," imeeleza tafiti hiyo.

XS
SM
MD
LG