Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:01

Mvutano mpya kati ya Marekani na China umefanya masoko ya Ulaya kutotabirika


Rais Donald Trump na Rais Xi Jinping
Rais Donald Trump na Rais Xi Jinping

Vita vya maneno kati ya Marekani na China vinavyo ongezeka juu ya chanzo cha mlipuko wa virusi vipya vya corona vimesababisha thamani ya hisa kwenye masoko ya Ulaya kuanguka wakati ikianza shughuli za biashara wiki hii.

Thamani ya kipimo cha hisa cha Paris CAC-40 imeshuka kwa zaidi ya asilimia 4 na thamani ya kipimo cha hisa cha Frankfurt DAX imepata hasara ya asilimia 3.6 katikati ya siku wakati biashara ikiendelea.

Wakati huo huo kipimo cha hisa cha thamani ya kipimo cha hisa cha Hong Kong, Hang Seng imeshuka kwa kiwango cha kustaajabisha cha asilimia 4 na ile ya hisa za Seoul, KOSPI ilipata hasara ya asilimia 2.6, wakati thamani ya hisa ya Sydney ilikuwa iking’ara katika kanda hiyo, kwa kupanda asilimia 1.4.

Masoko ya Japan, China na Thailand yalikuwa yamefungwa kwa ajili ya siku kuu katika nchi hizo.

Wawekezaji wana wasiwasi kuwa mvutano wa kibiashara kati ya nchi mbili zenye uchumi mkubwa kuliko nchi zote duniani zinakaribia kuanza upya kutokana na tuhuma za uongozi wa Trump.

Trump anadai kuwa virusi vya corona vilivyo gundulika katika mji wa kati wa Wuhan mwisho wa mwaka 2019 vilitokea kwenye maabara ya kutafiti kinga dhidi ya maambukizi ya virusi vinavyo wadhuru binadamu na wanyama, hata baada ya idara za ujasusi za Marekani kufikia uamuzi kuwa virusi vya COVID-19 haikutengenezwa na mtu wala haitokani na vinasaba.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo Jumapili aliishutumu Beijing kwa kuficha hali mbaya iliyokuwa ikiendelea juu ya virusi hivyo na kuendelea kuhodhi shehena za vifa vya matibabu. China imerejea mara kadhaa kukanusha tuhuma hizo.

Kwa upande wa mafuta, bei zimeshuka ambapo mafuta ghafi ya Marekani kwa kipimo cha West Texas ilikua dola 18.26 kwa pipa ikiwa chini kwa asilimia 7.6, wakati bei ya kimataifa ya mafuta ya Brent, inauzwa kwa dola 25.80 kwa pipa, ikiwa imeshuka kwa asilimia 2.4.

Bei ya mafuta zimeporomoka kutokana na masharti ya karantini yaliyowekwa duniani kote na kusababisha kutokuwepo mahitaji ya mafuta na hivyo mafuta kufurika katika soko. Pia imesababisha bei ya mafuta ghafi Marekani kufikia chini ya sifuri kwa pipa wiki mbili zilizopita.

Bei inapokuwa chini ya sifuri inamaanisha wazalishaji wa mafuta wanawalipa wanunuzi kuhamisha mafuta yao kutoka katika bohari yao kutokana na wasiwasi watashindwa kuwa na uwezo wa kuhifadhi mafuta mengine yanayoendelea kuzalishwa.

XS
SM
MD
LG