Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 04:59

Thamani za hisa katika masoko ya fedha Marekani zashuka


Wafanyabiashara wakiwa katika Soko la Hisa New York Jumatatu, Machi 16, 2020. (AP Photo/Craig Ruttle)
Wafanyabiashara wakiwa katika Soko la Hisa New York Jumatatu, Machi 16, 2020. (AP Photo/Craig Ruttle)

Thamani za hisa katika masoko ya fedha Marekani zimeshuka tena Ijumaa, pale wastani wa hisa za kipimo cha Dow Jones kikishuka kwa asilimia 2 na hisa za vipimo vya S&P 500 na Nasdaq-100 zikishuka kwa zaidi ya asilimia 2 baada ya kuongezeka kwa biashara siku mmoja kabla.

Huko Ulaya, thamani ya vipimo vya hisa vya London FTSE, Frankfurt DAX, Ujerumani na Paris CAC-40 vilianguka kwa zaidi ya asilimia 2 biashara ilipoanza mapema leo.

Huko Asia nako kipimo cha hisa cha Japan cha Nikkei kimepata hasara ya asilimia 2.84 na hisa za S&P/ASX zilishuka kwa asili mia 3.4 huku masoko mengine yaliwa yamefungwa kwa ajili ya sikukuuu ya Mei mosi.

Masoko yote ya Ulaya na Asia Ijumaa yalifuata muelekeo wa Wall Street hapo Alhamisi.

Licha ya kushuka huko kwa ujumla mwezi wa April unaonekana ulikuwa mzuri kwa masoko ya fedha kwani kipimo cha Dow kilishuhudia faida ya asilimia 12.7, huku kipimo cha S&P 500 kupata faida ya asilimia 12.5 ikiwa ni faida ya juu kabisa kwa mwezi tangu mwaka 1987 na ni muamala bora zaidi katika mwezi Aprili katika kipindi cha miaka 82.

Faida ya hisa za kampuni ya Nasdaq ya asilimia 15.5 kwa mwezi huo ni ya juu zaidi tangu mwaka 2000 na ni muamala bora zaidi kwa mwezi Aprili kwa kipimo cha teknolojia kilichorikodiwa.

XS
SM
MD
LG