Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:05

Uingereza : Brexit na kuanguka kwa kampuni ya Thomas Cook


Kampuni kubwa ya utalii nchini Uingereza, Thomas Cook, imeanguka baada ya kushindwa kupata ufadhili na hivyo kufutilia mbali safari za wateja wake zaidi ya 600,000.

Kampuni hiyo ambayo imekuwa katika biashara kwa zaidi ya miaka 178, ilikuwa imesema Ijumaa kwamba ilikuwa inatafuta dola milioni 250 za dharura, ili kuepuka kuanguka, na kwamba ilikuwa katika mazungumzo ya wikendi na wamiliki wake wa hisa pamoja na wafadhili ili kuepuka matatizo.

Mamlaka ya safari za anga nchini Uingereza, imesema ndege nne za kampuni ya Thomas Cook, zitasitisha safari zake, na wafanyakazi wake zaidi ya laki mbili katika nchi 16 watapoteza ajira.

Miezi kadhaa iliyopita, kampuni hiyo ilikuwa imeripoti kiwango kidogo cha watalii kutokana na mgogoro wa Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya (Brexit), kuwa mojawapo ya sababu zinazopelekea kuwa na deni kubwa.

Serikali ya Uingereza imesema kurejea kwa wateja wake 150,000 ambao sasa wapo nje ya nchi, ndio idadi kubwa zaidi katika historia ya nchi hiyo.

Hatua ya kurejea kwao imeanza hii leo na mamlaka ya safari za anga Uingereza, imesema imepanga kutuma ndege kadhaa kuwarejesha nyumbani katika shughuli itakayochukuwa muda wa wiki mbili.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC

XS
SM
MD
LG