Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:58

Uingereza yapata Waziri Mkuu mpya


Boris Johnson, Waziri Mkuu mteule wa Uingereza. June 22, 2019.
Boris Johnson, Waziri Mkuu mteule wa Uingereza. June 22, 2019.

Boris Johnson ameahidi kuiondoa uingereza kutoka Umoja wa Ulaya kabla wa mwisho wa mwezi Oktoba, kazi ambayo ilimshinda Theresa May na kusababisha kujiuzulu kwake kama waziri mkuu

Uingereza imepata Waziri Mkuu mpya baada ya Boris Johnson kumshinda mpinzani wake Jeremy Hunt katika uchaguzi wa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Theresa May kama kiongozi wa chama cha Conservative na waziri mkuu wa nchi hiyo.

Theresa May atajiuzulu rasmi kama Waziri Mkuu Jumatano na Johnson ataapishwa kuchukua nafasi hiyo. Kazi kubwa inayomkabili Boris Johnson itakuwa kutekeleza mpango wa Brexit kuiondoa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya lakini mkakati wake una wapinzani wengi.

Johnson ameahidi kuiondoa uingereza kutoka Umoja wa Ulaya kabla wa mwisho wa mwezi Oktoba, kazi ambayo ilimshinda Theresa May na kusababisha kujiuzulu kwake kama waziri mkuu. Johnson alikuwa kiongozi wa kura ya maoni iliyotaka Uingereza kuondoka Umoja wa Ulaya mwaka 2016. Alishinda uchaguzi wa Jumanne katika chama cha Conservative kwa kura 92,153 dhidi ya mpinzani wake Jeremy Hunt aliyekuwa waziri wa mambo ya nje ambaye alipata kura 46,656.

XS
SM
MD
LG