Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 02:46

May ajiuzulu rasmi uongozi wa chama chake


Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amejiuzulu kama kiongozi wa Chama cha Conservative Ijumaa na duru ya kwanza ya upigaji kura kumchagua mrithi wake ndani ya chama cha Conservative unatarajiwa kuanza wiki ijayo.

May alichukuwa madaraka mwaka 2016 kufuatia kura ya maoni ya kusitisha mahusiano na Umoja wa Ulaya (EU) na alitumia muda wake mwingi katika miaka mitatu akishughulikia mpango huo.

May ataendelea kuwa waziri mkuu hadi wabunge watakapomchagua kiongozi mpya wa chama hicho mchakato utakaochukuwa hadi miezi miwili.

Hata hivyo alishindwa mara tatu kuwashawishi wabunge kuunga mkono mpango wake wa kujiondoa Umoja wa Ulaya (Brexit).

Waziri mkuu atakaye chaguliwa atakuwa na kipindi kifupi chini ya miezi mitano kuamua iwapo arejeshe mpango wa May na kuchelewesha kujitoa umoja wa Ulaya (Brexit) kwa mara nyingine, au aondoke EU bila ya makubaliano yeyote.

Wagombea kadhaa kati ya kumi na moja ambao wanataka kuchukuwa nafasi ya May, akiwemo waziri wa mambo ya nje wa zamani Boris Johnson, wamesema wanampango wa kuomba kuwepo mabadiliko ya makubaliano hayo, pamoja na kuwa EU imesema haitaanzisha mazungumzo mara nyingine.

Duru za siasa zinaeleza kuwa May hatalihutubia taifa lakini anatarajiwa kuwasilisha barua ya kujiuzulu katika "Kamati ya 1922" ya chama chake.

Wachambuzi wanasema kuwa Boris Johnson anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kushinda.

Waziri Mkuu May alitangaza kujiuzulu Mei 24 baada ya kushindwa kufanikisha makubaliano ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya (Brexit)

XS
SM
MD
LG