Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:38

Ushawishi wa matumizi ya Benki za KIislamu waongezeka Afrika - Tafiti


Shirika la utafiti wa masuala ya kiuchumi na hisa Moody’s linaeleza kwamba mfumo wa kutumia benki za Kiislamu katika biashara umekuwa ukiongezeka kote duniani katika miaka ya hivi karibuni na hasa barani Afrika

Mfumo huu wa benki hutumia mali kama msingi wa kufanyia biashara, na haulipishi au kutoza riba na hauwekezi kwenye biashara zinazo fahamika kama haramu katika dini ya Kiislamu kama vile ya pombe, nyama ya nguruwe au kamari.

Mwandishi wa sauti ya amerika mjini Johnesburg anaripoti kuwa ukuaji wa benki za Kiislamu ni mkubwa huko Afrika Kusini ambako ni kitovu cha uwekezaji wa fedha barani Afrika.

Waislam wajiunga na benki za Kiislamu

Ripoti hiyo inaeleza kwamba Waislamu wengi wanaacha kutumia benki za kawaida na kujiunga na benki hizo za Kiislamu. Inaripotiwa kwamba baada ya Farhaan Mattiar kurithi duka la kuuza nguo za harusi liliko kwenye soko la kale la maduka ya wahindi mjini Johanesburg, aliamua kufanya mambo kwa njia tofauti.

Mattiar alimshawishi baba yake kuondoka kwenye mfumo wa kawaida wa benki na kujiunga kwenye mfumo mpya wa kiislamu. Anasema utaratibu umekuwa mwepesi kwa kuwa hata hakuhama kutoka benki ya zamani kutokana na kuwa benki nyingi kubwa nchini humo zinatoa huduma hiyo ya mfumo wa benki za kislamu. Ni mtindo unaokua kote barani Afrika

"Bado tunatumia benki ya zamani kwa kuwa bado tunahitaji mikopo kwa ajili ya kuendelea mbele, lakini kwa kubadili kidogo mambo kadhaa yataleta leta tofauti kubwa," amefafanua.

"Tofauti ni kwamba kwenye mfumo wa kawaida wa benki, ni kwa hakika namna wanakopesha fedha tofauti na beki za Kiislamu ambapo wanawekeza fedha kutokana na mapato yako. Hivyo upande moja ni faida kutokana na mapato na upande mwengine ni tozo la riba.

Mkuu wa mfumo wa benki ya Kiislam

Naye Mkuu wa mfumo wa benki wa Kiislamu kwenye benki ya First National ya Afrika Kusini Amman Muhammad anasema biashara imenawiri barani Afrika kutokana na ongezeko la Waislamu barani humo .

"Tunashuhudia ukuaji wa wastani na siyo kwa benki yetu ya FNB, lakini naamini pia hilo linafanyika kwenye mabenki mengine yanayotoa huduma hiyo, " ameeleza.

Muhammad anasema pia kuwa mfumo wa benki za Kiislamu unaweza kutoa faida kubwa kwa mataifa ya Kiafrika. Anazungumzia mafanikio ya hundi ya KIislamu ya thamani ya dola 500 za kimarekani iliyotolewa Afrika kusini 2014 chini ya mfumo huo maarufu kama sukuk.

Sukuk katika benki ya Kiislamu

Sukuk ni hisa katika benki za Kiislamu ambazo zimepangwa katika njia ambayo zinatoa faida kwa wawekezaji bila ya kukiuka sheria ya Kiislam ambayo zinakataza riba

"Kwa mara ya kwanza kabisa tunasikia serikali ya Tanzania ikizungumza kuhusu kutoa sukuk, pia tumesikia Kenya ikizungumzia kutoa sukuk.Nigeria nayo tunasikia inafuata mkondo huo. Naamini kuwa umaruifu wa hundi hizo na mafanikio yake yanaanza kuonekana, labda mataifa mengine mengi ya Afrika yataiga mfumo huo kuendeleza miundombinu yao," ametoa ufafanuzi.

Msimamo wa Mufti wa Afrika Kusini

Hata hivyo Siyo kila mmoja anaekubaliana na wazo hilo. Msomi wa kiislamu wa Afrika kusini Mufti AK ameambia VOA kuwa tofauti inayosemekana kati ya mfumo wa benki wa kiiskamu na ule wa kawaida inategemea unavyotazama kati ya riba na faida. Anawashauri wanafunzi wake dhidi ya mfumo huo.

Hakuna lolote la Kiislamu kwenye mfumo huo. Asilimia 90 ya watu wanaohusika wanatafuta dola katika mfumo huo. Wanacheza tu na maneno na kuchezea na akili za watu. Hilo ndilo linalofanyika.

Wanasihiwa kutumia benki ya Kiislamu

Mottiar kwa upande wake anasema kuwa anajaribu kuwarai wafanyabiashara wenzake waanze kutumia mfumo huo ingawa una gharama zake. Anasema kuwa yeye kama Muislamu anaamini kuna Baraka kila unapotenda haki. Anasema ni kutokana na hilo ndio anaamini kuwa mfumo wa benki wa kiislamu utakubalika katika siku zijazo.

Huku baadhi ya wafanyabiashara wa kiislamu wakieleza kuwa na shaka, wengine wanasema kuwa bado wanatafakari kuhusu mfumo huo. Wanasema iwapo wataweza kudumisha Imani yao na pia wapate fedha kwa wakati mmoja, basi kuna haja ya kufikiria kuhusu mfumo huo.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG