Licha ya kwamba matokeo ya utafiti huo ambapo kiwango cha maambukizi kilikuwa asilimia 14.4, bado kuna maeneo ambayo kiwango cha maambukizi yako juu, huku mkoa wa Kigoma na halmashauri zake nyingi zikiongoza kwa maambukizi.
Tathmini hiyo itaiwezesha Tanzania kufuatilia utekelezaji wa mpango wa kupambana na ugonjwa wa malaria ili kufikia azma ya kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030.
Wizara ya afya imetoa tamko kuwa, ugonjwa wa malaria ni kati ya maradhi yanayo sababisha vifo vingi nchini ambapo kwa mujibu wa takwimu za sasa, katika kila wagonjwa 1,000 wa malaria, 9 kati yao hufariki dunia na makundi ya jamii yaliyo katika athari kubwa ya malaria ni watoto na wajawazito.
Akizindua tafiti hiyo Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Mwalimu ametaja halmashauri ambazo kiwango cha maambukizi ya malaria bado kiko juu ni pamoja na Kakonko asilimia 30.8, Kasulu 27.6, Kibondo 25.8, uvinza 25.4, Kigoma25.1, Buhigwe 24, Geita 22.4, Nanyamba 19.5, Muleba 19.4, na Mtwara 19.1.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Peter Serukamba ameziomba halmashauri nchini kuhamasisha wananchi kutumia vyandarua vyenye dawa.