Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:19

Wataalamu waonya mlipuko mpya wa malaria


FILE - Juhudi za kukabiliana na malaria kwa kuboresha upimaji wa ugonjwa huo katika nchi ya Thailand, Novemba. 29, 2017.
FILE - Juhudi za kukabiliana na malaria kwa kuboresha upimaji wa ugonjwa huo katika nchi ya Thailand, Novemba. 29, 2017.

Baada ya miaka 16 ya mafanikio katika kutokomeza malaria, ugonjwa huo umeanza kuongezeka duniani, na wataalamu wanaonya kuwa kama hatua za kudhibiti hazijachukuliwa ugonjwa huo utaenea, na mafanikio yote hayo kuwa bure.

Vyanzo vya habari nchini Uingereza kwenye mkutano huo Jumatano, vinasema kuwa wajumbe wa mkutano huo wametoa wito kuongezewa fedha kwa programu hiyo inayopambana na malaria ulimwenguni.

Mmiliki wa kampuni ya Microsoft Bill Gates amechangia mabilioni ya dola za Kimarekani katika kukabiliana na ugonjwa wa malaria.

Msaada wake umesaidia sana katika kupunguza ugonjwa huo. Vifo vinavyotokana na ugonjwa huo vimepungua kwa asilimia 60 kati ya mwaka 2000 na 2015 ikiwa ni idadi ya uhai wa watu milioni saba waliookolewa kutokana na vifo vinavyosababishwa na malaria.

Wakati mkutano huo wa Malaria ukiendelea kando ya Mkutano wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola nchini Uingereza, Gates amewaambia wajumbe wakiwemo viongozi kadhaa wa Kiafrika, vita dhidi ya malaria lazima iimarishwe.

“Ikiwa hatuendelei na ubunifu tutarudi nyuma katika mapambano haya. Kama hatujasimama kidete kwa kutekeleza maamuzi tunayofanya hivi leo, malaria itaongezeka na kuuwa zaidi ya watoto milioni kwa mwaka kwa sababu dawa za kutibu na kuuwa vidudu vya malaria zimekuwa tayari hazina uwezo wa kukabiliana na tatizo hilo," ameongeza mfadhili Gates.

Ugonjwa wa malaria unakadiriwa kugharimu uchumi wa nchi za Kiafrika kwa zaidi ya Dola bilioni 12 kwa mwaka na zinatumia hadi asilimia 40 ya bajeti za afya za taifa. Watoto na wanawake wajawazito ndiyo wanao athirika zaidi na ugonjwa huu.

XS
SM
MD
LG