Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:28

Trump asema hakumfukuza kazi Comey


Kitabu cha Comey kikiwa tayari sokoni nchini Marekani.
Kitabu cha Comey kikiwa tayari sokoni nchini Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump amedai Jumatano kuwa hakumfukuza kazi Mkuu wa zamani wa FBI James Comey mwaka 2017 kwa sababu alikuwa akiongoza uchunguzi juu ya kuhusika kwa Russia na uchunguzi wa kampeni yake ya 2016, mgongano wa moja kwa moja unaokinzana na kile alichokisema baada ya kuondolewa katika wadhifa wake.

“Mbabaishaji James Comey, atajulikana kama Mkurugenzi dhaifu kuliko wote katika historia ya FBI, hakufukuzwa kwa sababu ya uchunguzi wa kubabaisha wa Russia japakuwa, hapakuwa na njama yoyote (isipokuwa ni Demokrats wenyewe)! Trump amesema katika ujumbe wake wa Twitter.

Baada ya Trump kumfukuza kazi Comey Mei 9, siku mbili baadae aliliambia Shirika la habari la NBC kuwa atamfukuza Comey katika hali yoyote, “akijua kuwa hakuna muda muwafaka kwa kufanya hivyo,” lakini alikuwa anafikiria uchunguzi unaofanywa dhidi ya Russia alipoamua kumfukuza.

“Nilipoamua kufanya hivyo, nilisema kuiambia nafsi yangu, ‘Unajua, suala hili la Russia linalofungamanishwa na Trump na Russia ni habari iliozushwa. Ni udhuru unaotolewa na Wademokrati kwa kushindwa uchaguzi ambao walitakiwa washinde,” Trump amesema.

Trump alikutana na waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergey Lavrov na balozi wa zamani wa Russia nchini Marekani, Sergey Kislyak katika White House May 10, chini ya siku moja baada ya kumfukuza kazi Comey, akiwaambia, " Hivi nimemfukuza mkuu wa FBI. Ni mpumbavu, hiyo ni kazi ovyo. Nilipata shinikizo kubwa kwa sababu ya Russia. Hiyo imeshaondolewa.

Trump ametoa maoni yake kuhusu kufukuzwa kwa Comey kutoka nafasi yake ya Idara ya makosa ya jinai (FBI) ambacho ni chombo cha juu katika kutekeleza sheria, wakati habari zake zilipokuwa zinavuma katika vipindi vya habari katika siku za karibuni akikinadi kitabu chake, "A Higher Loyalty."

Kitabu hicho ni simulizi yake mwenyewe juu ya maisha yake kama msimamizi wa sheria na maingiliano yake na Trump kabla ya kufukuzwa.

Comey amemkejeli Trump akisema kuwa "hana maadili ya kuwa rais", na kusema "siyo jambo la kawaida" kwa rais wa Marekani kutaka raia wa Marekani aingizwe jela, na Trump amesema Comey lazima atakuwa katika ujumbe wake mwengine wa tweet wiki hii.

XS
SM
MD
LG