Huku nchi mbali mbali zikiadhimisha siku ya Malaria ulimwenguni zilizofanyika Jumanne tarehe 25, mwezi Aprili mwaka wa 2017, shirika la afya duniani (WHO), lilitoa ripoti yenye takwimu zilizoonyesha kuwa visa vya malaria vimeshuka kwa asili mia 21 katika kipindi cha miaka mitano.
Kwenye hafla iliyofanyika mjini Nairobi mkesha wa kuamkia maadhimisho hayo, maafisa wa shirika hilo la kimataifa walisema kuwa licha ya kupungua kwa visa hivyo, bado asili mia 90 ya magonjwa yote ya Malaria duniani yako katika nchi za bara la Afrika, zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara.
Kufuatia hayo, Dr Charles Kamotho, anayemiliki taasisi ya The International Clinic mjini Thika, Kenya, na ambaye amekuwa akitibu wagonjwa wa Malria kwa muda mrefu, alizungumza na Sauti ya Amerika na kutoa tathmini yake kuhusu hali halisi ya ugonjwa huo katika taifa hilo la Afrika Mashariki.
Kadhalika alizungumzia jaribio la chanjo mpya ya Malaria linalofanyika katika nchi za Kenya, Malawi na Ghana, chini ya ufadhili wa WHO.
Daktari huyo alihojiwa na mwanahabari wa VOA, BMJ Muriithi: