Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 19:59

Burundi yatangaza malaria janga la kitaifa.


Mgonjwa akipatiwa dawa za malaria na mhudumu wa afya
Mgonjwa akipatiwa dawa za malaria na mhudumu wa afya

Watu 700 tayari wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa malaria nchini Burundi mwaka huu, ikiwa ni sawa na watu kumi kufa kila siku, na tayari serikali imetangaza kuwa malaria ni janga la kitaifa.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa Waziri wa Afya Daktari Josiane Nijimbere ametangaza Jumatatu kuwa kiwango cha dola za Kimarekani milioni 31 zinahitajika ili kukabiliana na ugonjwa huo.

Waziri huyo ametangaza kuwa ugonjwa wa malaria umekuwa ni janga la kitaifa.

Kulingana na takwimu kutoka wizara hiyo wananchi milioni mbili waliuguwa homa ya malaria tangu mwanzoni mwa mwaka 2016, hadi hivi sasa.

Waziri wa afya amelinganisha maambukizi ya mwaka huu na yale ya mwaka jana akisema kati ya wakazi milioni kumi nchini, watu milioni nane sawa na robo tatu ya wananchi waliumwa malaria mwaka jana.

Maambukizi yaliongezeka kwa asilimia 13 mwaka huu ukilinganisha na mwaka jana ambapo katika miezi miwili ya mwanzo, waliofariki dunia kutokana na malaria walikuwa theluthi moja ya waliofariki kwa kipindi cha mwaka mzima.

Mikoa inayoathiriwa zaidi ni pamoja na Muyinga Kirundo na Karusi kaskazini Ngozi na kayanza kaskazini mwa Burundi, pamoja na mkoa wa Ruyigi mashariki na karusi kati kati. Sababu za ugonjwa huo kuongezeka, ni mabadiliko ya hali ya hewa, amesema waziri.

Ameongeza kuwa kutokana na madiliko ya taibia nchi, sasa mbu wanao ambukiza ugonjwa huo wanaweza kupatikana katika nchi nzima.

Kadhalika katika mikoa hiyo joto limepanda sana. Kuna pia kilimo cha mpunga na kama mnavyojuwa vyote hivyo vinahitaji maji mengi.

Waziri amesema ni vuzuri kuendeleza kilimo hicho lakini tuna wakumbusha watu wasiache maji yakitiririka karibu na makazi yao ili mbu wasipate mahali pa kuzaliana na watu waendelee kutumia vizuri vyandarua.

Sasa mkakati umeandaliwa kwa ushirikiano na wahisani ili kukabiliana na ujonjwa huo na kiwango cha fedha kinachohitajika ni dola milioni 31 za kimarekani

Waziri wa afya imesema dawa za dharura zimekwisha nunuliwa na kwamba wako tayari kuwatibu raia pasipo kulipa gharama yoyote.

Wizara imesema waganga wa ziada walipelekwa kusaidia katika maeneo yalioathiriwa zaidi kukiwa na mpango pia wa kuwahudumia wananchi ambao wanaishi katika vijiji vilivyoko mbali na vituo vya afya.

Kwa mara ya mwisho ni mwaka 2002 ambapo ugonjwa huo wa malaria ulitangazwa nchini Burundi kuwa ni janga la kitaifa.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Haidallah Hakizimana, Burundi

XS
SM
MD
LG