Katika mahojiano yaliyotangazwa na kituo cha CNN mapema jumatatu, Conway amesema, “Kazi yangu sio kutafuta uthibitisho. Hilo ni jukumu la upelelezi.’
Alipoulizwa na mwendesha kipindi wa CNN Chris Cuomo, Conway hakusema iwapo White House itaweza kutimiza muda iliyopewa na Kamati ya Usalama ya Bunge la Marekani kupeleka ushahidi (Jumatatu) kuthibitisha madai ya Trump, ambayo aliyatoa kwa njia ya twitter zaidi ya wiki mbili zilizopita.
“Jawabu ni kuwa sina ushahidi wowote na nina furaha kuwa kamati ya usalama ya Bunge inachunguza hili,”Conway amekiambia kituo cha habari cha ABC katika kipindi cha “Good Morning America.” Baadae alituma ujumbe wa tweet kwamba uongozi “unaridhishwa” na uchunguzi unaoendelea kufanywa na bunge na utatoa maoni baadae.”
Wapinzani wa Trump wamemkosoa rais kwa kutoa madai yaliyo sababisha mtaharuki juu ya kurikodiwa simu. Alituma madai hayo kwenye akaunti ya Twitter bila ya ushahidi. Kurikodiwa kwa simu za raia wa Marekani kunahitaji ruhusa maalum kutoka mahakamani, na Trump kama rais anaruhusa ya kuweka wazi habari hizo za siri.
James Clapper, ambae alikuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa, amesema kuwa hakuna kitu kinachofanana na madai ya Trump kilichowahi kufanyika.
Pia mwezi huu, Wikileaks imetoa karibuni nyaraka 8,000 zikidai kutoa siri kuhusu vitendea kazi vinavyotumika na CIA kufanya udukuzi katika computer zilizokusudiwa, simu za mkononi na TV za kisasa.
Conway ametumia habari hizi zilizosambaa kuhalalisha madai ya Trump.
Hata hivyo mkurugenzi wa FBI, James Comey yeye binafsi ameihimiza Idara ya Sheria kukanusha madai ya Trump lakini yeye mwenye hajajitokeza kufanya hivyo.
Seneta John McCain, Mrepublikan mwenye ushawishi, amesema Jumapili: “Nafikiri rais lazima achague moja kati ya mambo mawili: aiondoe kauli yake au atoe taarifa zaidi kitu ambacho Wamarekani wanastahili kufahamishwa, kwa sababu, iwapo yule aliyemtangulia katika madaraka alikiuka sheria, Rais Obama alikiuka sheria, tuna jambo zito hapa, kwa kifupi,” seneta wa Arizona amesema.
Ombi la Kamati ya Usalama ya Bunge limetaka ifikishiwe ushahidi Jumatatu katikabarua iliyotumwa kwa Idara ya Sheria na mwenyekiti wa jopo, Mwakilishi Devin Nunes (R-Calif) na mwenzie Mwakilishi wa Demokrat, Adam Schiff (D-Calif), kwa mujibu wa afisa wa Bunge.
Msaidizi huyo hana ruhusa ya kuzungumzia ombi hilo kwa hivyo aliomba jina lake lisitajwe.