Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 16:27

Hong Kong yatangaza maandamano yanayoendelea ni tishio kwa usalama wa umma


Waandamanaji wakiwa wamefunika nyuso zao wakikiuka katazo la hivi karibuni la kufunika nyuso jengo kubwa lenye maduka ya biashara Hong Kong, Oct.13, 2019.
Waandamanaji wakiwa wamefunika nyuso zao wakikiuka katazo la hivi karibuni la kufunika nyuso jengo kubwa lenye maduka ya biashara Hong Kong, Oct.13, 2019.

Vikundi vinavyounga mkono harakati za demokrasia Hong Kong vimepunguza kufanya maandamano wikiendi, wakati maafisa wa serikali wakizidi kuvichambua vikundi vya waandamanaji hao kuwa ni tishio kwa usalama wa umma.

Polisi nchini humo wameendelea kuvilinganisha vikundi hivyo na uvunjifu wa amani unaofanywa na wanaharakati wenye mafungamano na ugaidi wa ndani ya nchi.

Kwa kipindi cha miezi minne iliyopita, Hong Kong imeyumbishwa kutokana na maandamano makubwa na ghasia dhidi ya kile kinachoonekana kuwa ni juhudi ya Beijing kunyang’anya madaraka na uhuru wa kiraia ambapo mji huo ambao unatawaliwa na China ulikuwa unafurahia mfumo wa nchi-mmoja- yenye tawala mbili.

Mvua wakati wa maandamano

Siku ya Jumapili ambapo mvua inanyesha, zaidi ya waandamanaji 1,000 walijipanga katika vibaraza vya maduka makubwa ya biashara katikati ya mji wa Hong Kong, wakiimba “pigania uhuru.”

Baadhi ya wanaharakati hao walikuwa wamefunika sura zao katika jengo kubwa lenye maduka ya biashara walisababisha usumbufu kwa mgahawa unaodhaniwa kumilikiwa na China kwa kutuma mamia ya maombi bandia wakiagiza chakula katika mtandao wa biashara za migahawa ya kieletroniki.

Katika makao makuu ya polisi kikundi cha wastaafu wanaoitwa “Silver-Haired Marchers” walikusanyika na kukaa wiki nzima makao makuu ya polisi wakiunga mkono maandamano yanayofanywa na vijana waliowengi.

Kikundi cha waandamanaji walikuwa wanatengeneza visanamu kwa kutumia karatasi katika sherehe zinazofanyika Kowloon, iliyoko nje ya kisiwa cha Hong Kong.

Lakini, mkutano uliokuwa unatarajiwa kufanyika katika wilaya yenye maduka ya biashara huko Causeway Bay hayakufanyika, ambako wiki iliyopita maelfu ya watu waliandamana katikati ya jiji hilo.

Polisi wa kuzuia ghasia walitupa mabomu ya machozi kuwalenga waandamanaji Jumapili katika eneo ambalo wiki iliyopita mwanadamanaji mmoja alipigwa risasi za moto.

Mwezi Juni, ushiriki katika maandamano dhidi ya serikali uliongezeka wakati takriban watu milioni 2 walipojitokeza kupinga muswada ambao hivi sasa umeondolewa bungeni uliokuwa unataka kuwarudisha wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu kufunguliwa mashtaka China bara ambapo wakosoaji wa muswada huo wanasema ungeipa serikali ya Beijing nguvu kubwa ya kuwakamata wakazi wa Hong Kong.

Mwenendo wa uhalifu

Wakati sehemu kubwa ya maandamano yalikuwa ya amani, kumekuwepo na ongezeko la matukio ya vurugu ambapo wanaharakati wanaofunika nyuso zao wamekuwa wakiharibu nyumba za biashara na mfumo wa usafiri wa chini ya ardhi wa jiji hilo, na kuwashambulia polisi kwa kuwatupia matofali na mabomu ya petroli yanayotengenezwa majumbani.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC

XS
SM
MD
LG