Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:04

Mataifa ya Afrika yataka UN iitishe mdahalo juu ubaguzi wa rangi


Mataifa ya Afrika yametuma barua kwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuliomba kuitisha kikao cha dharura kujadili ubaguzi na ukatili wa polisi.

Barua hiyo iliyosainiwa na nchi 54 imeandikwa na Balozi wa Burkina Fasoka katika Umoja wa Mataifa kwa niaba yao. Msemaji wa baraza hilo ameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP.

Katika barua hiyo Afrika inaliomba shirika hilo la UN kushughulikia masuala ya haki za binadamu kufungua mjadala wa dharura kuzungumzia ubaguzi.

Mjadala huo utaangalia ubaguzi unavyokiuka haki za binadamu, ukatili wa polisi dhidi ya watu wenye asili ya kiafrika na vitendo vya ukatili dhidi ya waandamanaji wanaoshinikiza kuondolewa kwa mfumo kandamizi na wakikatili wa polisi.

Ombi hilo linataka mjadala huo kufanyika wiki ijayo wakati baraza hilo litakaporejea kwenye kikao chake cha 43, baada ya kusitishwa kutokana na janga la COVID-19.

Hatua hiyo imekuja baada ya familia ya George Floyd, jamaa wa waathirika wa ukatili wa polisi pamoja na takriban mashirika yasiyo ya kiserikali 600 kuliomba baraza hilo kufungua mjadala wa dharura juu ya suala hilo.

Ili ombi kama hilo liweze kukubaliwa na baraza hilo, linahitaji kuungwa mkono na angalau taifa moja.

XS
SM
MD
LG