Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 05:34

Meya wa London ataka kifo cha Floyd kuhamasisha usawa kote duniani


Meya wa London Sadiq Khan
Meya wa London Sadiq Khan

Meya wa London Sadiq Khan amesema wiki hii kifo cha George Floyd kinabidi kumulika ukosefu wa usawa na ubaguzi wa rangi kote duniani.

Akitoa hoja juu ya ubaguzi huo amesema siyo tu uko Marekani na kwamba bado watu weusi huko London hadi leo hawana nafasi sawa na raia wengine.

"Na ndio muhimu tujielimishe juu ya tatizo hili na kufahamu kile kinachowafikia ndugu zetu weusi. Na kwa hakika ubaguzi wa rangi unatendeka kwa njia mbali mbali," ameeleza meya huyo.

Marekani

Wakati huo huo maandamano ya kutaka mageuzi katika mfumo wa polisi na sheria kandamizi pamoja na kukomeshwa ubaguzi wa rangi Marekani yanafanyika kwa amani kwa zaidi ya siku 10 sasa tangu kufariki kwa Mmarekani mweusi George Floyd alipokuwa anashikiliwa na polisi mjini Minneapolis.

Siku ya Alhamisi ibada ya kwanza kati ya tatu ilifanyika katika mji wa Minneapolisi na kuhudhuriwa na familia wanaharakati na maafisa wa serikali ya mji huo. Ibada ya maziko ya George Floyd yamepangwa kufanyika mjini Raeford, North Carolina Jumamlosi na maziko yatafanyika Jumanne.

Al Sharpton aahidi maandamano kuendelea

Kiongozi mkongwe wa kutetea haki za kiraia hapa Marekani Al Sharpton, amehidi kwamba maandamano ya wananchi yataendelea hadi “watakapofanikiwa kubadili kabisa mfumo wa sharia hapa nchini.”

Kiongozi huyo alisema hayo wakati zaidi ya watu 100 waliungana katika ibada ya maombolezi mjini Minneapolis kwa ajili ya George Floyd.

"Kile kilichomfikia Floyd kinatokea kila siku katika nchi hii yetu ikiwa ni katika huduma za elimu na afya na katika kila fani ya maisha ya Wamarekani. Wakati umefika kwa sisi kusimama kwa jina la George na kusema ondoa goti lako kwenye shingo letu," Al Sharpton mtetezi haki za kiraia Marekanialisisitiza.

Siku hiyo hiyo ya Alhamisi, maseneta wa chama cha Democratic katika bunge mjini Washington walikusanyika kuomboleza kwa ajili ya George Floyd. Seneta wa New Jersy Cory Booker, amesema wanatowa heshima zao kwa wale wote walouliwa na polisi hivi karibuni.

Cory Booker Seneta wa New Jersey alisema : Leo tumekusanyika hapa kwa maombolezi sio tu ya kifo cha kikatili, bali pia kutoa heshma kwa maisha yake George Floyd. Hivi sasa tunasita kwa dakika nane na sekunde 46 kumkumbuka George Floyd.

Maandamano yanaendelea kwa amani

Hiyo ilikuwa moja kati ya ibada mbali mbali inayofanyika hapa nchini wakati maandamano yanaendelea kwa amani na utulivu kukiwa na ghasia za hapa na pale katika baadhi ya miji, lakini si sawa na zilizoshuhudiwa wiki iliyopita.

Hapa Washington waandamanaji walikuta uzio mkubwa umewekwa nje ya White house kuwazuia kuingia kwenye uwanja maarufu wa la Fayette. Hata hivyo waandamanaji walibakia hapo hadi muda wa amri ya kutotoka nje kuanza saa tano usiku.

Maandamano yaungwa mkono duniani

Wakati maandamano yakiendelea hapa Marekani waandamanaji wamekuwa wakijitokeza katika mataifa mbali mbali kuanzia Australia ambako kwa wiki nzima wamekuwa wakiandamana na siku ya Alhamisi wakuu wa serikali wamejaribu kuzuia maandamano makubwa yanayopangwa kufanyika Jumamosi mjini Sydney, kwa madai ya hofu ya kuenea kwa virusi vya corona.

Waziri mkuu wa jimbo la New South Wale, Gladys Berejiklian, anataka mahakama kuu kutangaza maandamano hayo yanakwenda kinyume cha sheria.

Hayo yakiendelea maandamano yamendelea kufanyika Ijuma katika miji mbali mbali ya dunia, huko Asia waandamanaji wa Korea Kusini walikusanyika kudaia haki kutendeka kwa ajili ya Floyd. Wakati wakazi wa Beirut, Lebanon na Ukanda wa Gaza, watu waliwaunga mkono wamarekani katika kutaka kukomeshwa ubaguzi wa rangi.

XS
SM
MD
LG